Paroko
wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Enduimet,Jimbo Kuu la Arusha,Padri Pius
Shao(katikati)akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuzalisha
Umeme kwa nguvu za Jua ,kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusambaza
Teknolojia(KAKUTE),Livinus Manyanga na Afisa Elimu Sekondari wilaya ya
Longido,Gerson Mtera.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kusambaza Teknolojia(KAKUTE),Livinus Manyanga akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuzalisha Umeme kwa nguvu za Jua katika
hospitali ya Kanisa Katoliki,Parokia ya Enduimet wilaya ya Longido mkoa
wa Arusha,mtambo huo umegharamiwa na Wakala wa nishati Vijijini(REA)na
wadau wengine.
Paroko
wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Enduimet,wilaya ya Longido Jimbo Kuu la
Arusha,Padri Pius Shao akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa
kuzalisha Umeme kwa nguvu za Jua uliogharamiwa na Wakala wa nishati
Vijijini(REA)na wadau wengine.
Hospitali
ya Kanisa Katoliki Parokia ya Enduimet,Jimbo Kuu la Arusha imekabidhiwa
Mtambo wa nishati Jua wenye uwezo kuzalisha 10 KW ,uliofadhiliwa kwa
pamoja kati ya Wakala wa Nishati Vijijini(Rea) na serikali ya Ujerumani
kwa lengo la kuiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma za afya kwa wananchi
wanaozunguka eneo hilo.
Mkurugenzi
wa Hospitali hiyo,Padri Pius Shao alisema kuwa kabla ya mradi huo wa
kutumia nishati Jadidifu kuanza walikua wakitumia Genereta dogo ambalo
lilikua haliwezi kukidhi mahitaji ya hospitali jambo ambalo lilikua
kikwazo katika utendaji kazi kwani halijaunganishwa na Gridi ya taifa.
Alisema
kutokana na kiwango cha umeme wanachopata wanakusudia kuanza huduma za
upasuaji mwezi huu,hatua itakayowapunguzia gharama wagonjwa kwenda mbali
kutafuta huduma hizo.
“Mtakumbuka
wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuja kuongoza harambee ya ujenzi
wa hospitali hii mwaka 2012, tulimwomba gari la kubeba wagonjwa tayari
limeshafika na linatoa huduma hiyo kwenye vijiji
vinavyotuzunguka,tutazidi kutafuta fedha zaidi kuhakikisha tunapata
huduma bora za kiafya kwa wananchi wetu ili waweze kufanya shughuli za
kuwaletea maendeleo,”alisema Padri Pius
Awali
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusambaza Teknolojia(Kakute)iliyofunga mitambo
hiyo,Livinus Manyanga alisema mradi wa kufunga mtambo wa kufua wa jua
kwaajili ya kuboresha huduma ya afya kwenye hospitali ya Enduimet ni
matokeo ya shindano la kubuni miradi ya kuendeleza nishati vijijini
linalotolewa na REA kila baada ya miaka miwili na kufadhiliwa na Benki
ya Dunia.
Alisema
fedha zilizotekeleza mradi huo ni ruzuku ya Sh 146 milioni kutoka
REA,serikali ya Ujerumani ilitoa kiasi cha Sh 121 milioni na wadau
wengine kiasi cha Sh 38 milioni zilizofanikisha mradi huo kwenye jamii
ya wafugaji.
Manyanga
alisema kuwa malengo ya mradi huo mbali ya kuweka mtambo katika
hospitali hiyo pia umewaunganishia umeme wa mkopo nafuu familia 100
ndani ya vijiji vya Kamwanga,Lerangwa na Olmolog.
No comments:
Post a Comment