Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
(kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. Gullamhussein S.
Kifu (katikati) wakati wa ziara ya kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa
vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya
Bw. Laurean Masele na anayefuata ni Kaimu Afisa Vijana Halmashauri ya
Wilaya ya Mbarali Bw. Athuman Mustafa Kinza.
Mkuu
wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akiwaelekeza vijana
wa Mbarali namna ya kuandika andiko la mradi wakati wa semina ya
Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
iliyotolewa kwa vijana wa Mbarali hivi karibuni.
Mwenyekiti
wa Kikundi cha Wood Works Bw. Stafford Gwimile (wa pili kulia)
akizungumza na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo walipotembelea mradi wa kikundi hicho kwa ajili ya kutathmini
shughuli za vijana na utoa ushauri kwa vijana wa Wilaya ya Mbarali Mkoa
wa Mbeya.
Maafisa
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na vijana
wa Kikundi cha Umati Sanaa Group wakiburudika na muziki uliokua
ukitumbuizwa na vijana wa kikundi hicho wakati wa ziara ya kutembelea
vikundi vya vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya.
Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
(waliokaa kushoto) akizungumza na vijana wa Umati Sanaa Group wanaofanya
kazi za sanaa walipofika kuangali kazi zinazofanywa na kikundi hicho
wakati wa ziara ya uhamasishaji kwa vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mbarali Mkoa wa Mbeya.(Picha zote na: Genofeva Matemu – Mbarali, Mbeya)
No comments:
Post a Comment