Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto)
akisalimiana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo
Januari 27, 2015(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto)
akisaini katika kitabu cha wageni mapema leo alipowasili Makao Makuu ya
Jeshi la Magereza kwenye ziara ya mafunzo kuhusu uendeshaji wa Jeshi la
Magereza(kulia) ni Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji,
Deonice Chamulesile.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwasilisha mada
yake ya uchokozi kuhusu Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele
ya Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi
Tanzania(hawapo pichani).
Wakufunzi
kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika
uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa
Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza,
Ukonga Dar es Salaam.
Wanafunzi
Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia
mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto
katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la
Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Kamishna
wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki
kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya
mafunzO(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania,
Meja Jenerali GS Milanzi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Bregedia
Jenerali Sylivester Minja.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).
No comments:
Post a Comment