Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome
Sijaona(Katikati) akikata utepe, kuashilia uzinduzi Rasmi wa nyumba
aliyokabidhiwa Salome Mhando ambaye alitelekezwa na mume wake baada ya
kujifungua watoto mapacha mfurulizo hadi kufikia sita na kukosa Mahali
pa kuishi, Covenant Bank imemkabidhi nyumba hiyo ambayo ataimiliki yeye
mwenyewe pamoja na thamani za ndani na Bima ya Matibabu kwa Mwaka mzima.
Anaeshuhudia ni mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja (wa
kwanza kushoto) na Salome Mhando (wa kwanza kulia).
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona
(kushoto), Pamoja na Mkurugenzi wa benki Hiyo, Sabetha Mwambenja,
wakimkabidhi hati ya kiwanja na Umiliki wa nyumba Salome Mhando, Mama
alietelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo,
hadi kufikia sita, Benki hiyo imemkabidhi nyumba hiyo pamoja na Bima ya
Matibabu kwa mwaka mzima.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome
Sijaona(Katikati) akiwapokea watoto wa Salome Mhando wakati akiwasili
kukabidhiwa nyumba yake. Pamoja nae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant
Bank, Sabetha Mwambenja na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Margaret
Kyarwenda.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona (wa
kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha
Mwambenja na Mama Salome Sijaona, Wakimfurahia moja wa watoto wa mama
huyo akipanda katika moja ya vitanda walivyokabidhiwa.
Baada
ya kujifungua watoto mapacha mfululizo na kufuatiwa na kitendo cha
kutelekezwa na mume wake huku akiwa hana sehemu ya kuishi, Hatimaye
Salome Muhando amenunuliwa na kukabidhiwa nyumba na Covenant Bank
ambayo ataishi yeye na watoto wake.
Salome
, mwenye watoto sita mapacha alitelekezwa na mume wake baada ya
kujifungua mapacha mara tatu mfululizo na kusababisha kukosa sehemu
maalum ya kukaa yeye pamoja na watoto wake ambapo baada ya kutelekezwa
msamaria mwema alijitolea kumhifadhi katika shamba lake lililopo eneo la
Mabwepande.
Baada
ya kusikia kilio cha mama huyo kupitia vyombo vya habari Covenant Bank,
ilijitolea kumnunulia nyumba mama huyo ambayo ataimiliki yeye moja kwa
moja na kumpatia mtaji wa biashara ambao utamsaidia kuenesha maisha yake
ya kila siku.
Akizungumza
na waandishi wa habari, punde baada ya kukabidhi nyumba hiyo Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Balozi, Salome Sijaona, amesema
baada ya kuona mateso ambayo mwanamke huyo amekuwa akiyapata kwa kukosa
makazi , Chakula na mahitaji mengine ya kibinaadamu waliona ni vyema
benki yake kujitolea kumsaidia ikiwa ni katika sehemu moja ya kutimiza
majukumu yake ndani ya jamii.
“Tumeguswa
sana na mateso ambayo amekuwa akiyapata Bi. Salome Mhando, yeye pamoja
na watoto wake baada ya kutelekezwa na mume wake kwa kigezo ha kuzaa
watoto mapacha mfurulizo, tuliguswa na kuamua kujitolea kumnunulia
nyumba ambayo ataimiliki yeye mwenyewe.” Alisema Balozi, Sijaona na
kuongeza kuwa.
“Nyumba
hii tumemkabidhi pamoja na samani za ndani ya nyumba ambazo
zitamuwezesha sasa kuishi maisha ya amani, na furaha akiwa kama wanawake
wengine na kufurahi pamoja na watoto wake.”
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja amesema kuwa pamoja
na kumkabidhi nyumba mama huyo pia Benki hiyo, imempatia Bima ya
Matibabu kutoka AAR ambayo itamsaidia kupata Matibabu yeye pamoja na
watoto wake wote.
“Pamoja
na kumpatia nyumba Salome pia tunampatia Bima ya Matibabu ambayo
itamuwezesha yeye na watoto wote kutibiwa katiba Hopitali zote zilizo
mahali popote nchini, Tuna uhakika sasa atakuwa na uhakika wa afya yake
na watoto wake katika kipindi chote hivyo atakuwa na nafasi ya kufanya
shughuli zake za uzalishaji kwa amani., Alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa
Upande wake Salome , aliwashukuru Covenant Bank kwa kujitolea kumsaidia
na sasa ana uhakika wa maisha yeye pamoja na watoto wake.
“Ninawashukuru
sana Benki ya Covenant kuniwezesha kumiliki nyumba yangu ninawashukuru
sana na ninaomba waendelee na moyo huo wa kuwasaidia kina mama wenye
matatizo kama haya kwa sababu siko peke yangu,” alisema na kuongeza,
“Kina
mama tumekuwa na wakati mgumu sana katika ndoa zetu hususai katika
masuala ya uzazi, Ninawashukuru watu wote ambao walijitolea kunisaidia
chakula na nguo katika wakati wote ambao nilikuwa sina sehemu maalum ya
kukaa, hadi sasa ninamiliki nyumba yangu. Alihitimisha Salome.
No comments:
Post a Comment