Rais
wa TFF Bw. Jamal Malinzi pia aliambatana na Viongozi mbalimbali hapo
Uwanjani akiwemo Bw. Pelegrinius A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji
ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF
makao makuu, Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni Kiongozi
kamati ya Waamuzi Nchini.
Doron
Mommsen(kushoto) akiongea na Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi(kulia) jana
wakati Rais huyo alipotembelea kujionea Ukarabati huo wa Uwanja wa
Kaitaba ambao Utachukua Muda wa Miezi Mitatu. Meneja wa Mradi Bw. Doron
Mommsen amemweleza Ndugu Jamal Malinzi kwamba Ukarabati unaendelea
Vizuri na kinachoendelea kwa sasa ni kusawazisha Udongo katika Uwanja
huo.
Meneja
wa Mradi Bw. Doron Mommsen akishukuriwa na Rais Jamal Malinzi Uwanjani
hapo Kaitaba baada ya kumwelezea kwa kirefu katika Ujenzi huo wa Uwanja.
No comments:
Post a Comment