Saturday, January 24, 2015

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ASHUHUDIA KUSAINIWA KWA MAKUBALIANO YA MWENDELEZO WA KAMPENI ZA USALAMA BARABARANI BAINA YA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA,JESHI LA POLISI NA VODACOM TANZANIA

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa kwanza toka kushoto) akishuhudia kutiwa saini kwa makubaliano ya kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani baina ya Baraza hilo na kampuni ya simu za mikooni ya Vodacom Tanzania. Akitia saini kwa naiba ya Baraza ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa pili toka kushoto) na kwa niaba ya Vodacom ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa kwanza toka kushoto) akihakiki waraka wa makubaliano ya kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani baina ya Baraza hilo na kampuni ya simu za mikooni ya Vodacom Tanzania. Akitia saini kwa naiba ya Baraza ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa pili toka kushoto) na kwa niaba ya Vodacom ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa kwanza kulia) akikabidhiana na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa nne toka kulia) waraka wa makubaliano ya kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani baina ya Baraza hilo na kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania waliousaini kwa niaba ya Baraza na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa tatu toka kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo ya Baraza, Henry Bantu (wa pili toka kulia).
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa kwanza kulia) pamoja na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa nne toka kulia) wakionyesha waraka wa makubaliano ya kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani baina ya Baraza hilo na Vodacom Tanzania waliousaini kwa niaba ya Baraza na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa tatu toka kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo ya Baraza, Henry Bantu (wa pili toka kulia).

No comments: