Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bibi Ester Makalili
akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kukutana na vijana wa
Wilaya hiyo kutoa mafunzo ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.
Kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi Ester Riwa na kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda
Mbeya Bw. Laurean Masele.
Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
akitoa mada ya Ujuzi kwa vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi
za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya
Chunya Mkoa wa Mbeya.
Afisa
Ushirika kutoka Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Bw. Mwanyi Magambo
akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Chunya umuhimu wa kuunda Saccoss ya
Vijana itakayowawezesha vijana kuweka akiba na kukopeshana wakati wa
semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana jana katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.
Afisa
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga kushoto akizungumza na wanakikundi wa Ngozi
group wanaosindika ngozi kwa njia ya asili na kutengeneza bidhaa za
ngozi kwa kutumia ngozi walizosindika walipowatembelea kukagua mradi wao
jana katika kijiji cha Mkwajini Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Wa pili
kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
Kijana
Meshaki Ngailo kushoto kutoka kikundi cha Vijana Bush Man Works
kinachofanya kazi ya kuunga vyuma akizungumza na maafisa waliofika
kukagua mradi wa kikundi chake wakati wa ziara ya kukagua miradi ya
vijana wa Mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment