Mfanyabiashara na mmiliki wa duka
la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth mshana akiongea na
Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma ya kufanya malipo
kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field Communication (NFC) based
solution ya Airtel Money. kadi hii maalum inamuwezesha mteja kufanya
malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa maalum tu mara moja, kisha
kuweka nambari ya siri na kufanya malipo mahali popote. kwa sasa huduma
hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Huduma hii ya Near Field
Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha kadi na kifaa tu kupitia
huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na
kampuni ya simu za mkononi ya airtel
Mama elizabeth mshana mmiliki wa
duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa kupitia kadi huduma iliyozinduliwa
na Airtel mkoani Arusha inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa
haraka zaidi kwa kutumia kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye
teknolojia ya Near Field Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa
na Airtel Money.akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde.
Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha
kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za
mkononi ya airtel.
Afisa uhusiano wa kampuni ya simu
za mkononi ya AIRTEL Jane Matinde akimuelekeza Moja ya wateja bi Merry
Ngowi jinsi ya kutumia kifaa na kadi maalumu ambacho hutumika
kukamilisha miamala ya malipo katika maduka mbalimbali. Huduma hii
ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya
mitandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya
airtel, tukio lifanyika mwishoni mwa wiki mkoani arusha eneo la muromboo
wakati wa uzinduzi huduma hiyo ambayo inaleta njia salama, ya haraka na
rahisi kwa wateja kufanya malipo.
Mfanyabiashara wa duka la chakula
katika eneo la Mrombo Arusha Bwana Elibariki Ngowi akipokea malipo
kutoka kwa mteja kwa kupitia kadi maalum ya Near Field Communication
(NFC) ya Airtel Money. , huduma imezinduliwa na Airtel mkoani Arusha
inawawezesha wateja wake kufanya malipo kwa kutumia kadi hiyo maalumu
kwa haraka bila huanza kupiga *150*60# hii unagusisha tu na kulipa
haraka kati kanti ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akishudia
huduma hiyo inavyofanya kazi. Huduma hii ya Near Field Communication
(NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza
kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkononi ya airtel.
No comments:
Post a Comment