Friday, July 15, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKABIDHI POWER TILLER 102 ZILIZOTOLEWA NA MBUNGE WA MBARALI MHE HAROUN MULLA KWA AJILI YA VIJIJI NA MITAA 102 ...

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amepokea Power Tiller 102 zenye Thamani ya Shilingi Milioni 510 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mh. Haroun Mulla kwa ajili ya shughuli za Kilimo na Kijamii kwa Vijiji na Mitaa 102 ya Jimbo la Mbarali
Akikabidhi msaada huo mbunge wa jimbo hilo amesema kuwa Wilaya ya Mbarali ni Wilaya ya Kilimo na Ufugaji hivyo Msaada wake umelenga kusaidia Vijiji na Mitaa ili kuchochea Vijiji na mtaa kuwa na chanzo cha Mapato na pia kuchochea Kilimo
Akipokea kabla ya kuzikabidhi Power Tiller hizo kwa Viongozi wa Vijiji na Mitaa amemshukuru na kumpongeza Mbunge kwa msaada huo Mkubwa na kwa kufanya hivyo ametekeleza vizuri ilani ya Chama Tawala ya kuongeza ajira akiamini hizo Power Tiller zitaendeshwa na Madereva na wasaidizi na pia zitaongeza ukuaji wa Uchumi
Aidha amewataka Viongozi wa Vijiji kuzitunza na kueleza kwa wananchi Mapato yatakayopatikana kutokana na hizo Power Tiller Alisema " Siyo hizi Power Tiller ziwe Mali zetu ni Mali za Kijiji mzitumie vizuri na tuache fitna maana kuna wengine wangetamani badala ya Powe Tiller mngepewa Fedha hapa nasema Mbunge katupa nyavu tukavue Samaki nawatakia kazi njema na Mipango Mizuri"
Amewataka wananchi wote kufanya kazi na muda kwa vijana kucheza pool haupo na hivyo halmashauri zote zitenge asilimia 5 mapato ya ndani kwa ajili ya Mikopo ya Vijana na akina Mama
Power Tiller 102 zenye Thamani ya Shilingi Milioni 510 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mh. Haroun Mulla kwa ajili ya shughuli za Kilimo na Kijamii kwa Vijiji na Mitaa 102 ya Jimbo la Mbarali Mkoani Meya.

No comments: