Tuesday, September 8, 2015

ZOEZI LA KUGAWA CHAKULA LAENDELEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA...

Wakimbizi kutoka nchini Burundi  walioko katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Byesige Josephat (anayemimina mafuta) na Hezron Mtangirwa(kushoto), wakimbizi kutoka Burundi waliohifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wakipima mafuta ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana ,baada ya kugawiwa mafuta na Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia chakula (WFP), ambalo lina kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. 
 Kinamama wakimbizi toka Burundi wakipata mgao wao wa unga unaotolewa kwa wakimbizi wanaohifadhiwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.  Serikali kwa kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa imeendelea kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa toka Burundi wanapata chakula cha kutosha kwa ajili ya mahitaji yao.
Mkimbizi Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) baada ya kupokea mgao wa chakula unaotolewa na  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililo  na Kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Kushoto ni mtoto wake aitwaye Nsengiyumva Idiphonce.

No comments: