All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, September 6, 2015

ACACIA YAIDHAMINI STEND UNITED KWA KITITA CHA BILLIONI MOJA....

   
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazo zitumia katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom.
Mwenyekiti wa stand united Amani Vicent (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini wa timu hiyo na Makamu wa rais wa ACACIA anaeshugulikia masuala ya Kampuni, Deo Mwanyika mara baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazotumia msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali na wadhamini wao kampuni ya ACACIA.
Baadhi ya wachezaji wa Stend United wakiwa na baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Acacia ambao ni wadhamini wa timu hiyo muda mfupi mara baada ya kuzindua rasmi jezi za timu hiyo zitakazotumika katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza tarehe 12.09.2015.
Baadhi ya wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazotumia msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom wakati walipokuwa wakizionyesha kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(Hayupo pichani wakati wa utiaji saini wa mkataba wa timu hiyo na kampuni ya ACACIA.
Baadhi ya Viongozi wa Acacia kutoka kulia ni Alex Lugendo (Meneja wa Uhusiano na Serikali wa ACACIA), Elias Kastra – (Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa Bulyanhulu)na Nector Foya - (Meneja wa Mawasiliano wa ACACIA) wakifuatilia mchezo kati ya Stend United na Olympic Stars ya Burundi Mchezo uliopigwa katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.
Baadhi ya washabiki wa Stend United waliohudhuria wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu hiyo ikiwa pia ni sehemu ya kusherekea udhamini wao na kampuni ya Uchimbaji wa madini ya ACACIA.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi yao itakayokuwa ikitumika kwa michezo ya uwanja wa nyumbani na ile ya ugenini wakati wa msimu wa ligi kuu ya Vodacom.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazo zitumia katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazo zitumia katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom.

RC wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akipokea jezi ya timu ya stend United kutoka kwa makamu wa rais wa ACACI, Deo Mwanyika.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mguu mkoa wa Shinyanga Benasta Lugola akipokea jezi ya timu ya stend United kutoka kwa makamu wa rais wa ACACI, Deo Mwanyika.
Mashabiki wa Stend United waliojitokeza kusherekea udhamini wa timu yao katika uwanja wa Kambarage.
Wachezaji wa Stend United wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo.
Timu za Olympic Stars yenye jezi ya bluu na timu ya Stand united yenye jezi ya rangi ya dhahabu zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo wao wa kirafiki.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisalimiana na Kapteini wa timu ya Olympic Stars ya Burundi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisalimiana na kapteni wa timu ya Stand United Nassoro Masoud “CHORO”
Makamu wa rais wa Acacia anaeshughulikia masuala ya Kampuni Deo Mwanyika akisalimiana na kapteni wa timu ya Stand United Nassoro Masoud “CHORO” wakati timu hiyo ilipoumana na Olympic Stars ya Burundi.
Kikosi cha Stend United Kilichoshiriki mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya Olympic Stars ya Burundi katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga. Mchezo huo uliisha kwa ushindi kwa timu ya Stend United Kushinda 1-0.
Kikosi cha Olympic Stars cha nchini Burundi kilichochuana vikali na Stend United ya Shinyanga Tanzania.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini  aliyekuwa Shinyanga.
 KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Acacia iliingia mkataba wa miaka miwili na timu ya Stend United ya Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kushiriki ligi kuu ya Vodacom ambayo inategemewa kuanza tutimua vumbi katikati ya mwezi huu. Stand United ni moja kati ya timu bora kabisa katika kanda ya ziwa ambayo imeshiriki katika ligi kuu msimu uliopita 2014/2015 na kumaliza ikiwa nafasi ya tisa.
Udhamini wa ACACIA katika misimu hii miwili ya ligi kuu itasaidia katika kuifanya timu ya Stand United iweze kufanya vizuri katika michezo yake, pamoja na kusaidia katika kuboresha programu mbalimbali za timu na kuendeleza vipaji pamoja na masuala ya Utawala.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Makamu wa rais wa Acacia aneshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, amesema  “Kwa takriban mwaka mmoja, tumekua tukifanya kazi pamoja na Stand United. Kwa muda huo tulianzisha mchakato wa kutambua namna nzuri ya kuboresha ushirikiano wetu ili kunufaisha watu wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Bwana Deo amesema Msimu uliopita uliwapatia fursa nzuri ya kushuhudia uwezo wa timu hiyo hasa ukizingatia ilikua mara yao ya kwanza kushiriki ligi kuu, “Baada ya tathmini ya kina, tunadhani huu ni muda muafaka wa sisi kusaini makubaliano au mkataba wa kuidhamini na kufanya kazi pamoja ya kuikuza timu hii ya nyumbani maarufu kama “Chama la wana”.
Hivyo, Leo, Acacia tunasaini mkataba na timu ya Stand United kwa udhamini wa misimu miwili ya ligi kuu, wenye thamani ya Shilingi bilioni moja. Udhamini huu unajuamuisha shughuli za uendeshaji wa timu, kuboresha uongozi na kukuza vipaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent, amesema udhamini huo wa miaka miwili utakuwa chachu kwa timu yake kufanya vizuri katika ligi kuu, “Msimu uliopita tulimaliza tukiwa nafasi ya nane na kipindi hicho hatukuwa na fedha ya kutosha kuendesha timu, lakini kwa udhamini tulioupata kutoka kwa ndugu zetu wa Acacia vijana wetu safari hii watafanya vizuri zaidi.
Kampuni ya Acacia ni kampuni inayoongoza kwa shughuli za uchimbaji wa madini hapa Tanzania huku ikiwa na Migodi mitatu katika kanda ya ziwa, kupitia mradi wa “Acacia Maendeleo Fund” ambao ndio pia umetoa udhamini wa timu ya Stend umekuwa pia ukitekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Jamii hapa nchi huku kampuni hiyo ikieleza kuwa dhamira yake ni kuendelea kufanya kazi na Jamii zinazowazunguka katika kuwaletea Maendeleo wenyeji.

No comments: