Saturday, September 12, 2015

TASWIRA MBALIMBALI ZA MTANANGE WA MBEYA CITY NA KAGERA SUGAR AMBAPO KAGERA WALIIBUKA KIDEDEA KWA KUWATUNUKU GORI MOJA KWA BILA MBEYA CITY FC NYUMBANI....

Kikosi kazi cha Timu ya Mbeya City fc kikiongwozwa na Gorikipa mahiri Juma Kaseja katika Maombi kabla ya kuanza Mtanange, ambapo Kagera Sugar iliibuka mshindi kwa kuitundika Mbeya City fc Gori Moja kwa bila (1,0) Dakika ya 41, Mchezaji Poul Ngaiyoma Jezi Nambari 8, Mgongoni kuipatia ushindi Timu ya Kagera Sugar katika Mechi ya Kwanza Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mtanange ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mtanange ukiendelea katika Uwanja wa Kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya ambapo Kagera Sugar iliibuka kidedea kwa Gori moja kwa Sifuri (1,0) Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.
Juma Kaseja Jezi Nambari Moja Mgongoni akiwa makini Lango la Mbeya City katika Mtanange wa Mbeya City fc na Kagera Sugar, ambapo Kagera Sugar iliibuka kidedea kwa Gori moja kwa Sifuli (1,0).
Mashabiki wa Mbeya City fc wakishangilia katika Mtanange uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kagera moja huku Mbeya City fc Mama kajabwela Tumbo kamsokota Tumbaku Bilaaa..

No comments: