All Right Receved by MR.PENGO 2016

Saturday, May 16, 2015

LOWASSA ATIKISA ARUSHA,ACHANGISHA ZAIDI YA SH,MIL 200 ,KUTANGAZA NIA MEI 24 MWAKA HUU.

SAM_2715
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2723Umati mkubwa wa wananchi wa Arusha wakiwa wanampungia mkono Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee 
SAM_2688
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh mkuu wa Bakwata mkoani  Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika hafla ya harambe ya ujenzi wa  msikiti wa Patandi iliyofanyika jana katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana.
SAM_2682Mkurugenzi wa kituo cha Redio 5 Arusha Francis Robart akiwa anawasilisha jumla ya fedha zilizopatikana katika harembee hiyo kwa Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa.
SAM_2709Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa  msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee 
?????????????
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anasalimiana na baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
SAM_2716Taswira ya picha wakati Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anaondoka katika uwanja wa msikiti mkubwa jijini Arusha
SAM_2727
?????????????
Msafara wa pikipiki 
SAM_2695Mgombea anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris  akiwa anasalimiana na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa baada ya kumkabidhi shilingi Milioni sita kwaajili ya ujenzi wa msikiti Patandi.
SAM_2693Diwani Mathias Manga  akiwa anawasilisha mchango wa rafiki yake wa karibu Husein Gonga wa shilingi Milion saba.
SAM_2679Mkurugenzi wa Redio 5 Arusha Francis Robart  kulia wakiwa wanapiga hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana
SAM_2730Muonekano jiji la Arusha
SAM_2660Kada maarufu wa chama cha CCM,Violet Mfuko katikati akiwa na diwani viti maalum Vick Mollel wakiwa wanamshangilia mgeni rasmi Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo 

SAM_2669Kushoto ni mtia nia jimbo la Arumeru mashariki Solom Sioi pamoja na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima wakifatilia jambo katika harambee hiyo

SAM_2673Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba akiwasilisha mchango wake

SAM_2672
SAM_2665Wananchi wakiwa wanamsikiliza Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa

Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo Mei 24 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.

Lowasa,alitoa kauli hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha sh,200 milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24 mwaka huu anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono siku hiyo.

"Niseme neno nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo nitahitaji mniunge mkono "alisema Lowasa

Lowasa kwa kujiamini aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja uwanja huo na kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.

"Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini"alisisitiza Lowasa 

Hatahivyo,Lowasa aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya Askofu wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu kusimamia amani ya mkoa huo.

Aliipongeza kamati hiyo na kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko jambo lolote kwa kuwa Arusha ni mji ambo ni chanzo cha utalii duniani.

"Tuendelee kuheshimiana bila kujali misingi ya dini,kabila au rangi lakini niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa kitalii bila amani hakuna utalii Arusha"alisema Lowasa na kuibua shangwe
Post a Comment