Friday, May 15, 2015

RAIS KIKWETE KWENYE SHEREHE ZA KILELE YA WIKI YA ELIMU.

 Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015. 
 Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwanafunzi Agatha Julius Ninga kutoka Shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora akiwa ni miongoni mwa wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika mitihani ya sayansi ya kidato cha nne mwaka jana 2014.Agatha alifanya vizuri katika somo la Biolojia.Rais Kikwete alitoa zawadi kwa wanafunzi, shule,halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa kumaliza Elimu ya msingi na elimu ya sekondari.Tuzo na zawadi hizo zilitolewa leo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu nchini.
Waziri wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa akitoa tuzo maalum kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu kitaifa iliyofanyika mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wanafunzi Maria Sagasii na Neema Harry kutoka Shule ya msingi ya Ignatius ya mjini Dodoma wakionyesha viungo vya ndani vya mwili wa binadamu somo la Biolojia katia banda la maonyesho katika Uwanja wa michezi wa Jamhuri wa mjini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu leo.
 Baadhi ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 .PICHA ZA FREDDY MARO, IKULU.

No comments: