Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Mbeya city wakoma kumwanya wakishangilia ushindi wa gori 2,1 kwa kuibugiza timu ya Yanga leo katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga wameshindwa kufurukuta mbele ya Mbeya City baada ya kukubali kipigo cha goli 2,1 dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Sokoine jijini Mbeya. Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi kwa timu ya Mbeya City kupata goli dakika ya sita kupitia kwa Hassan Mwasapili ikiwa ni mpira wa adhabu uliopigwa nje ya 18 na Kenny Ally kuaindikia goli la pili ikiwa nalo ni adhabu ambalo lilileta utata baada ya mwamuzi kulikataa na kisha kulikubali. Kutokana na hali hiyo wachezaji wa Yanga walianza kuliandama goli la Mbeya City na katika dakika ya 45 ya kipindi cha Kwanza Donald Ngoma anaiandikia Yanga goli la kufutia machozi ambalo lilidumu mpaka kipindi cha mwisho.
Na katika mchezo mwingine timu ya Simba imejihakikishia kuendelea kukaa kileleni baada ya kuoata ushindi wa goli 10 dhidi ya Stand United baada ya mshambuliaji wao Shiza Kichuya kuiandikia timu hiyo goli la uushindi kwa mkwaju wa penati. baada ya matokeo hayo Simba imeendelea kujikita kileleni kwa alama 35 nyuma ya alama 27 za mabingwa watetezi Yanga.
Mchezaji kutaka timu yaYanga Kelvin Yondani jezi Nambari 5 mgongoni akidhadhiana na muamuzi katika Mtanange wa Mbeya city na yanga Uwanjani Sokoine Jijini Mbeya..
Tuambieee Hilo ni Goriiii au sio Goriii....
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.
No comments:
Post a Comment