MBUNGE
wa Viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),UPENDO
PENEZA amesema kuwa ni uamuzi mzuri uliochukuliwa na kampuni hiyo kwani
mkoa huo umekithiri kwa mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu hivyo
ni ishara kubwa ya kuelekea kukombolewa.
Peneza
alisema kuwa anaamini watu wakimpenda Mungu wataacha kufanya mauaji ya
vikongwe na albino na watu wa kawaida, kwani mkoa huo unaongoza kwa
mauaji ya aina hii.Alisema Tamasha hilo ni msaada mkubwa kwa mkoa huo
kwani litahamasisha na kupinga mauaji huku akisisitiza kuwa kampuni ya
Msama ambayo inasifika kusaidia jamii anaiomba pia iwafikie hata watoto
wa mitaani wa mkoa wa Geita.
“Tunamshukuru
Msama na kamati yake kwani Tamasha linaweza kuwa msaada mkubwa kwa mkoa
wetu mauaji yamezidi si kwa walemavu wa ngozi na vikongwe hata watu wa
kawaida wanauwawa kwa mapanga na vitu vingine” alisema Peneza.Alitolea
mfano wa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Chadema, Alfonce
Mawazo aliyeuwawa kwa kukatwakatwa mapanga hivyo kupitia tamasha la
pasaka litawaasa waache mauaji.
“Kupitia
hili Tamasha naamini wataacha vitendo hivyo kwa sababu Mungu anasema
tusiue, mpende mwenzio, kwa hiyo mimi nadhani tamasha hili liwe la
kihistoria kwa ajili ya kuwataka na kumrudia mungu,” anasema. Peneza
alisema asiwe Msama tu hata asasi, kampuni na wadau mbalimbali
wajitokeze kupinga mauaji kwani hilo ni janga la kitaifa.
No comments:
Post a Comment