Wednesday, March 9, 2016

NMB MDHAMINI MKUU WA MKUTANO MKUU WA ALAT TAIFA.

NMB Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT taifa.
Benki ya NMB imekabidhi hundi ya mfano ya shilingi Milioni 100 kwa uongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa ALAT taifa unaotarajia kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Aprili Mjini Dodoma.
Fedha hizo ni kwaajili ya kugharamia gharama za mkutano mkuu unaotarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 400 kati yao wakiwa mameya 180 kutoka halmashauri zote nchini, wakurugenzi wa halmashauri wapatao 180, wawakilishi wa mikoa na wizara mbalimbali ambao jumla yao wanafika zaidi ya 400.

NMB imekuwa ikidhamini mikutano ya ALAT kila mwaka na kwa mwaka huu, malengo makubwa ni kuhakikisha halmashauri zote zinaingia kwenye mfumo wa malipo ya kielektroniki ili kuzuia upotevu wa mapato. NMB kama mpokeaji mkuu wa malipo kwa njia za kielektroniki kwenye halmashauri, tayari imeshafanya majaribio ya kupokea malipo kwa njia hizo na hivi karibuni itaanza kutoa huduma hiyo kwenye halmashauri zote nchini.
Kupitia mtandao wake wa matawi 180 nchini, NMB imekuwa karibu na wananchi wa halmashauri mbalimbali kwa kutoa huduma za kifedha na pia kusaidia serikali katika uboreshaji wa njia za ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki.
 Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 100 kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Habraham Shamumoyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mawasiliano-ALAT, Seif Hassan. NMB imedhamini mkutano mkuu wa ALAT unaotarajia kufanyika mapema mwezi April mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Habraham Shamumoyo akiongea na waandishi wa habari (hawako kwenye picha) kuhusu Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa utakaofanyika jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB - Richard Makungwa.

No comments: