Na Sultani Kipingo
Floyd Mayweather ameibuka mshindi katika pambano la karne baada ya kumdunda Manny Pacquiao kwa pointi nyingi alfajiri ya leo huko Las Vegas, Marekani.
Mmarekani Mayweather, 38, ametumia mbinu za hali ya juu za kujihami dhidi ya mpinzani wake Mfilipino, akifanya marekebisho muhimu kwenye raundi za awali kabla ya kupotea ulingoni.
Mayweather, ambaye ameongeza taji la WBO la uzito wa welterweight juu ya mataji ya WBC na WBA aliyonayo, alipewa ushindi kwa majaji watatu kuamua kapiga 118-110, 116-112 na 116-112.
Kwa ushindi huo, Mayweather amedhihirisha yeye ni bondia bora wa ngumi-kwa-ngumi wa zama hizi. Bingwa huyu anayeshikilia mataji matano sasa hajashindwa katika mapambano 48 katika miaka 19.
Akiwa bingwa wa mataji sita, Pacquiao, 36, anaishia ushindi wa mapambano 57, kapigwa mara sita na droo mbili.
Tiketi kwa mpambano huo wa karne ziliuzwa kwa dola £232,000 na mashabiki wa Marekani walicha dola 66 kuangalia kwenye luninga - kama ilivyokuwa duniani kote.
Floyd Mayweather
Bondia wa Kimarekani,Floyd Mayweather Jr akimrushia konde kali mpinzani wake, Manny Pacquiao wa Philipines wakati wa mpambano wao wa kihistoria na uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na watu wengi Duniani kote, uliopigwa mapema leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani. Bondio Floyd Mayweather ameshinda mchezo huo kwa point 118-110, 116-112, 116-112 kutoka kwa waamuzi wa mchezo huo na kunyakuwa mkanda wa WBC huku akiifanya rekodi yake ya kutopigwa kufikia michezo 48.
Mchezo ulikuwa ni mkali sana na Mabondia wote walikuwa wakirushiana makonde kwa zamu.
haya angalieni wenyewe hasa wale wanaosema jamaa kabebwa.
Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wakifurahi pamoja mara baada ya mpambano wao wa kihistoria uliopigwa mapema leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani.
Bondia Floyd Mayweather Jr akiwa na mikanda yake na tuzo aliyoshinda katika michezo mbali mbali
|
No comments:
Post a Comment