Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL umetangaza kusitishwa huduma za safari ya treni abiria kuanzia leo Ijumaa Machi 06, 2015 kufuatia eneo la tuta la reli kati ya stesheni za Kilosa na Kidette kuharibika kwa mafuriko ya mvua inayonyesha hivi sasa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakifanya tathmini ya jinsi zoezi la ukarabati utakavyofanyika na kwa muda gani.
Ikifafanua zaidi taarifa imeeleza kuwa tathmini ya mafundi hao ndiyo itakayoamua huduma hiyo ya usafiri wa treni za abiria itarejea lini.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya kwa niaba ya
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Mkurugenzi Mtendaji –TRL
Dar es Salaam
Machi 06, 2015
No comments:
Post a Comment