Friday, March 6, 2015

PSPF YASAIDIA KITUO CHA KULEA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, VINGUNGUTI JIJINI DAR.

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akipena mikono na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahama, wakati akikabidhi msaada wa mifuko ya saruji tani 3 na mabati, kwa ajili ya ujenzi kwenye kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu, cha Lukema. Hafla ya kukabidhin msaada huo kwa kituo hichomnkinacholea watoto 70, ilifanyika Ijumaa Machi 6, 2015. Kushoto ni mwenyekiti wa kituo hicho, Fatuma Ramadhani. 

Baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho wakisubiri kukabidhiwa msaada huo

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akiteta jambo na mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu cha Lukema, kilichoko Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam Ijumaa Machi 6, 2015. Mfuko huo umetoa msaada wa saruji na mabati kwa ajili ya kupanua ujenzi wa kituo hicho kinacholea watoto 70 kwa sasa

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akizungumza jambo wakati alipofika kutoa msada wa saruji na mabati kwa niaba ya Mfuko huo kwa kituo cha kulea watoto waishio katika mazingira magumu, kituo cha Lukema, Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Machi 6, 2015.

Mwenyekiti wa Kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu cha Lukema, kilichoko Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Fatuma Ramadhani, akizungumza kwenye hafla ya kupokea msaada wa saruji na mabati vilivyotolewa na Mfuko huo kwa ajili ya ujenzi.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahame, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano. Kulia ni mkurugenzi wa kituo, Lukondo Mchundo 


Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (aliyechuchumaa katika), na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vingungjuti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahame, (aliyesimama kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto hao

No comments: