Mkurugenzi
wa Idara ya Asia na Australasia (wa kwanza kushoto), pamoja na Konseli
Mkuu wa Tanzania nchini Dubai Bw. Omar Mjenga wakifuatilia kwa makini
mazungumzo kati ya Mh. Membe na Askofu Wilson (hawapo pichani)
Picha na Reginald Philip
=================================================
Waziri Membe atoa rai kwa madhehebu
kuwaombea viongozi kuwa waadilifu
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa
rai kwa waumini wa Kanisa la Waadiventista Wasabato nchini kushiriki
kikamilifu katika kutengeneza viongozi bora wa Serikali wanaozingatia
misingi ya uadilifu, upendo na unyenyekevu.
Waziri
Membe ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya kufunga Kongamano la
Kimataifa la Utume la Kanisa la Waadventista Wasabato lililofanyika
katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2015.
Mhe.
Membe alisema kuwa Dini na madhehebu yanayo nafasi kubwa katika kujenga
jamii yenye maadili na hofu ya Mungu wakiwemo viongozi na hivyo
kupelekea taifa kuwa na amani, upendo na mshikamano. Alieleza kuwa kama
Waziri wa Mambo ya Nje, amejifunza kuwa diplomasia na hofu ya Mungu
vikifanya kazi pamoja hakuna changamoto yoyote isiyoweza kukabiliwa.
“Dini
na Diplomasia vina husiana pale masuala ya amani, ulinzi na usalama
yanapoguswa. Hivyo nawaomba mshiriki katika kutengeneza viongozi bora
katika jamii zetu kwa misingi ya uadilifu ambao watasimamia amani na
kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo rushwa,” alisema Mhe. Membe.
Aidha,
alilipongeza Kanisa hilo kwa kuwa mfano mzuri wa ustahimilivu na
uvumilivu wa kidini hapa nchini. Alieleza kwamba kamwe hajawahi kusikia
Kanisa la Waadiventista Wasabato limeingia katika mgogoro na Serikali,
dhehebu au dini nyingine na hilo ni funzo kubwa kwa Watanzania, kwamba
kutofautiana kiitikadi, kidini, kikabila au rangi si sababu tosha ya
kuwagombanisha na kuvuruga amani ya nchi.
“Nalipongeza
Kanisa lenu kwa kuwa mfano mzuri wa uvumilivu wa kidini na imani,
mnaendesha mambo yenu kwa uvumilivu mkubwa na kushirikiana na dini zote
na hili linatufundisha kuwa kutofautiana kwetu sio sababu tosha ya
kugombana” alisisitiza Membe.
Pia,
Mhe. Membe alilihakikishia Kanisa hilo dhamira ya Serikali ya kuendelea
kushirikiana nalo kwa ajili ya ustawi wa nchi na kufafanua kuwa
Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa dini zote kama
inavyoelezwa kwenye Katiba ya nchi. “Serikali inao wajibu wa kusaidia
dini na madhehebu kufanyakazi kwa uhuru. Bahati nzuri Katiba
inayopendekezwa imezingatia kulinda uhuru huo hivyo tuiunge mkono”
alifafanua Waziri Membe.
Vilevile
alilisifu Kanisa hilo kwa kuanzisha miradi ya huduma zikiwemo Shule15
za Sekondari na Msingi, Chuo Kikuu na Hospitali mbili ambavyo vinatoa
mchango mkubwa kwa Serikali na Wananchi kwa ujumla.
Awali
akimkaribisha Waziri Membe kufunga Kongamano hilo, Rais wa Baraza Kuu
la Makanisa ya Sabato Duniani, Askofu Ted Wilson alisema kuwa anawaombea
Viongozi wa Tanzania waendelee kuwa na maono kwa ajili ya kuwatumikia
wananchi na kwamba wakimtumaini Mungu atawawezesha kupata maono mapya
kwa ajili ya kulitumikia Taifa hili.
Kwa
upande wake, Mwenyeji wa Mkutano huo, Mchungaji Blasius Luguri
aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani ambayo imepelekea Tanzania
kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo ulioyashirikisha Mataifa
zaidi ya 20. Aidha, alimwomba Mhe. Membe kufikisha ujumbe kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wana imani na Tanzania kuwa ni nchi
ya amani, usalama na utulivu.
Kanisa
la Sabato ni Kanisa linalokua duniani likiwa na Waumini milioni 307
huku Waumini milioni 30 wakiwa Afrika na takriban milioni 5 wakiwa
Tanzania.
-Mwisho-
|
No comments:
Post a Comment