Sunday, February 8, 2015

NAPE ATEMBELEA MAGAZETI YA TANZANIA DAIMA NA JAMBO LEO.



Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akikutana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, leo akiwa katika ziara katika vyombo vya habari ambayo aliianza jana, jijini Dar es Salaam.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana kwa furaha na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Nevile Meena alipowasili kwenye kampuni hiyo leo akiwa katika ziara kwenye vyombo vya habari mjini Dar es Salaam


Nape akizungumza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima leo jijini Dar es Salaam


Nape akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za gazeti la Jambo Leo, leo mjini Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept inayochapisha gazeti hilo, Teophil Makunga.


Nape akiwa katika mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Jambo Concept


Nape akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo na uongozi wa Jambo Concept

Nape akimuonyesha Makunga Kalenda ya CCM ya mwaka huu (2015) kabla ya kumkabidhi kama zawadi.


Nape akimkabidhi zawadi ya kalenda ya CCM, Makunga


Baadhi ya waandishi wa habari katika chumba cha habari cha magazeti ya Jambo Leo


Nape akiwa kwenye chumba cha Breaking news cha magazeti ya Jambo Leo


Nape akiagana na mpigapicha mkuu wa Jambo Leo Richard Mwaikenda mwishoni mwa ziara katika chumba cha habari cha magazeti hayo. Picha na Bashir Nkoromo na Adam Mzee.

No comments: