Sunday, March 12, 2017

KAMATI YA UTALII WATEMBELEA YALIYOKUWA MAFICHO YA MWALIMU NYERERE WAKATI WA HARAKATI ZA UHURU MKOANI MBEYA, IJUE HISTORIA YA MTAA WA "SOKO MATOLA"JIJINI MBEYA.

Kamati ya Utalii ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikiongozwa na Afisa Utalii wa Jiji Bi.Levina Modest na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Geofrey Kajigili wanaofanya kampeni hii kabambe ya utambuzi wa Vivutio vyote vilivyopo Jijini Mbeya kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali za Uyole Cultural Tourism Enterprise pamoja na Elimishawamemtembelea Mzee Mkongwe wa Siasa nchini, Mzee Rashid Ally Sinkala ambaye amewahi kuwa Diwani wa iliyokuwa ikiitwa Kata ya Soko Matola (sasa Kata ya Maendeleo) kwa miongo kadhaa pia amewahi kutumika kama Meya ya Halmashauri ya Mbeya Mjini.Mzee Sinkala ameiambia Kamati ya Utalii kuwa Miaka zaidi ya 50 iliyopita wakati wa Siasa za Ukombozi wa Tanganyika Enzi za Chama cha Tanganyika African National Union (TANU)Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akifikia kwenye nyumba ya mwanasiasa Mkongwe mwanamke aliyejulikana kwa majina ya Zaituni Binti Matola.
Binti Matola alitenga chumba kimoja nyumbani kwake kama Maficho ya Mwalimu Nyerere.
Mzee Sinkala akiwa mlangoni mwa Chumba maalum alipokuwa akifikia Mwalimu Nyerere ndani ya nyumba ya muasisi wa TANU na mwanamke mashuhuri Hayati Zaituni Binti Matola aliyepelekea maeneo hayo kuitwa "Soko Matola" Jijini Mbeya
Wajumbe wa Kamati ya Utalii Jijini Mbeya wakimsikiliza kwa makini Meya mstaafu wa Halmashauri ya Mbeya Mjini Mzee Sinkala ndani ya nyumba ya kihistoria ya Binti Matola.
BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

No comments: