Monday, March 13, 2017

COCA-COLA KWANZA YAKAMILISHA SHANGWE NA WADAU WA COCA-COLA MKOWANI MBEYA.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios (kulia),  akigongesha soda ya Coca-Cola na viongozi wengine wa kampuni hiyo  kuashiria uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji hicho mkoani  Mbeya mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha (kutoka kushoto) ni David  Karamagi - Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Nalaka Hettiaratchchi –  Mkurugenzi wa Mauzo wa Coca-Cola Kwanza na Gary Pay – Meneja Mkuu wa  Coca-Cola Kwanza Mbeya. Sambamba na uzinduzi wa muonekano mpya, Kampuni  ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa zake mkoani Mbeya  ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia teknolojia ya kisasa   katika kiwanda chake kilichopo Mbeya. Picha zote na Mr. Pengo - MMG-MBEYA.

Akiongea wakati wa  hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios,  alisema  upanuzi na kufunga mitambo ya kisasa zaidi katika kiwanda cha  Coca-Cola mkoani Mbeya umefanyika  wakati muafaka ambapo umeenda  sambamba na mkakati wa kujiiimarisha zaidi katika soko la Mkoa huo na  maeneo yote ya Nyanda za Juu Kusini na kuhakikisha bidhaa zake  zinapatikana kila mahali na wakati wowote lengo likiwa ni kuwawezesha  wakazi wa Mbeya kufurahia ladha murua ya kinywaji cha Coca-Cola na  bidhaa nyingine zinazozalishwa na kampuni.
“Kampuni ya  Coca- Cola inayo historia ya kuwepo mkoani hapa kwa  muda mrefu, na  tumeona ni vyema tukawashirikisha katika mkakati wetu wa mafanikio wenye  lengo la kuongeza tija na ufanisi, ambapo tumeboresha kiwanda chetu na  pia tumejipanga kusambaza bidhaa zetu kuhakikisha zinawafikia wananchi  kwa urahisi na  mkakati huu tutautekeleza katika mikoa yote vilipo  viwanda vyetu”. Alisema Bwana Gadzios.
Wageni waalikwa waliofika kusherekea muonekano mpya wa kinywaji cha Coca-Cola.

No comments: