All Right Receved by MR.PENGO 2016

Wednesday, February 15, 2017

NAMAINGO YATOA ELIMU KWA WANANCHI WA KATA YA MAANGA MTAA WA MAENDELEO JIJINI MBEYA...

Kampuni lisilo la kiserikali "Namaingo Business Agency" ukanda wa Mbeya leo katika Kata ya Manga ,mtaa wa Maendeleo limefanya mkutano wa mafunzo kwa wananchi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani wakiwa na malengo makuu ya Kuifundisha jamii mbinu mpya na bora katika kuyaendea mafanikio binafsi na kupunguza utegemezi.
Akiongea kwa umaridadi mkubwa Bw.Gaudence Rwabyoma juu Pichani ambaye ni Mkufunzi wa masuala ya Uchumi ndani ya Namaingo ameutanabaisha Umma kwa kutumia mifano mtambuka kuwaeleza makumi ya wananchi waliokuwepo mkutanoni hapo mbinu mpya ya kufikia maendeleo hasa kwa kutumia mfano wa jinsi gani Serikali, mkulima, mnunuzi, taasisi za kifedha, mtaalamu na mwanasheria wanavyoweza kutegemeana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuzalisha zaidi.
Mkufunzi huyo ameutanabaisha Umma kuwa wao kama Namaingo wanafanya kazi kwa kushirikiana zaidi na serikali hivyo ni nafasi ya wananchi kukipatia maeneo mengi ya ardhi ya kuanzisha Vijiji mradi kwa kupata ekari nyingi za uwekezaji, pia Namaingo kuhakikisha wananchi wanapata mitaji kwa riba nafuu na masoko pia.
Wazee wa Mtaa wa Maendeleo kata ya Maanga wakifuatilia Semina elekezi iliyokuwa ikitolewa na Wakufunzi wa Namaingo Jijini Mbeya
Viongozi waandamizi wa Mtaa wa Kata ya Manga Jijini Mbeya wakiwa na Mratibu wa Namaingo Mkoa wa Mbeya (wa kwanza kulia) Bw.Jottam Willson
Elimu kwa vitendo Baadhi ya wakazi wa Kata ya Manga wakionyesha jinsi Namaingo inavyofanya kazi kwa kuwaunganisha Serikali,Wakukima/wafanyabiashara, wanunuzi, taasisi za kifedha,wataalamu na wanasheria.
PICHA NA MR.PENGO.
MAELEZO  NA THOBIAS OMEGA

Post a Comment