All Right Receved by MR.PENGO 2016

Wednesday, February 15, 2017

SHULE YA MSINGI SINDE YAPIGWA KUFULI KUTOKANA NA KUBOMOKA KWA CHOO CHA WANAFUNZIShule ya msingi Sinde iliyopo mtaa wa kagwina katika kata ya Sinde Jijini Mbeya imefungwa ghafla kutokana na Choo cha wanafunzi zaidi ya 1,600 kutitia na kubomoka hali iliyopelekea wanafunzi kukosa huduma ya choo shuleni hapo.

Mkuu wa Shule ya Msingi Sinde Mwl. Angomwile Mwanansyobe amesema kuwa Kutokana na janga hilo Jiji pamoja na Uongozi wa Shule uliamua kuifunga shule kwa kipindi cha majuma matatu ili kupisha Ujenzi wa vyoo hivyo na madarasa ya mitihani tu yaani Darasa la nne na darasa la saba ndio pekee wataendelea kusoma hapo shuleni kwa kutumia vyoo vya shule jirani ambazo zinapakana kwa ukaribu zaidi.
Mwl Mwanansyobe amesema,....."Kama Uongozi wa shule tunajua ni kwa jinsi gani taaluma kwa wanafunzi waliopo majumbani hivyo sisi kama walimu tutaitumia likizo fupi ya mwezi machi kuendelea na vipindi. 
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sinde Bw.Angomwile Mwansyobe akizungumzia kuhusu kufungwa kwa Shule na changamoto zilizowakumbuka
 Kina Mama ni jeshi kubwa,Hivi ndivyo inavyoonekana pichani huku wanafunzi kadhaa wakishuhudia wazazi wao wakichapa kazi kwa kujitolea
PICHA NA MR.PENGO
MAELEZO NA TOBIAS OMEGA
Post a Comment