Monday, July 18, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKABIDHI VITANDA 250 SHULE YA SEKONDARI IYUNGA AWAASA WANAFUNZI NA WANAJUMUIYA IYUNGA KUDHIBITI SHULE KUUNGUA MARA KWA MARA...

Leo ilikuwa siku ngumu kwa watendaji wa jiji la Mbeya na Veta pale Mkuu wa Mbeya Amos Makalla alipofanya ziara ya kuongea na Wanajumuiya ya Iyunga kuhusu udhibiti wa kuungua kwa Mabweni mara kwa mara shuleni wakati wote wakiamini hiyo ndiyo ajenda kumbe Mkuu wa mkoa ana taarifa kibao kuhusu wanafunzi kulala chini na kwamba vitanda 250 vilivyotengenezwa Veta kwa ajili ya Shule hiyo vimezuiliwa veta kwa madai ya shilingi milioni 70. Ghafla wakati anakaribishwa kuingia ukumbini aliwaambia twendeni kwenye Mabweni na mambo yalikuwa hivi.  
"Mkuu wa Shule nipeleke mabweni ambayo wanafunzi WANALALA chini, kwanini wanafunzi WANALALA chini?" Ndipo mwalimu Mkuu alipofunguka kuwa Vitanda havijaletwa Ndipo Mkuu wa MKOA aliagiza ndani ya Saa moja Vitanda viletwe na kaimu Mkurugenzi kuagizwa alipe deni hilo kwa awamu ndani ya Mwezi Mmoja kwani ni aibu kukaa Semina na Vikao wakati wanafunzi Wanalala Chini na kweli ndani ya Saa moja vitanda vililetwa na sasa tatizo la vitanda Iyunga Sekondari limetatuliwa 
Aidha amewataka wanafunzi kuhakikisha mabweni yao hayaungui tena na kila mwanafunzi awe Mlinzi wa Mwenzake

Baadhi ya Wana funzi wa Shule ya Sekondari Iyunga wakiwa katika ukumbi wa Shule hiyo wakifuatilia kwa Makini kikao kinachoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makalla hayupo Pichani.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akielekea katika Mabweni ya Wanafunzi wanao lala Chini kabla ya kugawa Vitanda hivyo..

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akizungumza mbele ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iyunga, Waandishi wa Habari sambamba na Wadau wa Elimu Mkoa wa Mbeya.

No comments: