Tuesday, July 5, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDA HILL PATAKAPO CHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI YAITWAYO NIOBIUM, KABLA YA KUANZA UCHIMBAJI KAMPUNI YACHANGIA MADAWATI 400 KWA MKOA WA MBEYA.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla wapili kulia atembelea Mradi wa Mgodi wa Madini katika kata Ya Songwe eneo la Panda Hill unaomilikiwa na Kampuni ya Panda Hill Tanzania Limited, ulioanza kufanya tafiti zake Mwaka 2013 juu Ya Ugunduzi wa Madini aina Ya NIOBIUM yanayotumika kwa Matumizi Ya Utengenezaji Ndege, Meli, Madaraja Makubwa duniani, Kompyuta, na Magari, Hapo awali utafiti wa Kuwepo kwa Madini haya hapa Tanzania ulianza Mwaka 1950.
Akizungumza na Wananchi pamoja na waaandishi wa habari juu ya Mgodi huu wa kwanza hapa Afrika kuzalisha Madini haya na ya Nne Duniani Mh.Rc.Makalla awapongeza Mgodi wa Panda Hill Tanzania Limited kwa kuchangia Madawati 400 katika shule zinazozunguka Mradi huo Pia na kuendelea kuchangia Maendeleo ya jamii mengine wakiwa tu katika utafiti kabla ya kuanza Uzalishaji ambao utaanza ndani ya Miezi 18 toka sasa na Kukamilika 2018 ambao utakua ukizalisha Tani Elfu tatu kwa siku
Mh.Rc.Makalla amewapongeza Panda Hill Tanzania Limited kwa uwekezaji huo utakaozalisha Ajira watu 500 ambao Mradi mzima uwekezajiwake ni Bilioni 500.

Sehemu ya Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Panda Hill Tanzania Limited.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla wapili kulia Akipongeza juu ya ya uchangiaji wa Madawati 400 kwa Mkoa wa Mbeya Yenye Thamani ya Milioni 22 kutoka katika Kampuni ya Panda Hill Tanzania Limited..
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akizungumza na Vyombo Mbalimbali vya Habari vilivyo hudhuria katika Mgodi huo wa Panda Hill  Songwe.

No comments: