All Right Receved by MR.PENGO 2016

Wednesday, July 6, 2016

KIJIPU EPELEEE:MOJA YA TAA ZILIZO WEKWA MAFIATI MATAA JIJINI MBEYA YAPIGWA NGWALA...

Huu ni Muendelezo wa Matukio Madogo Madogo yanayo endelea Kujitokeza katika eneo la Mafiati Mataa Jijini Mbeya ambapo ndipo Sehemu pekee kati ya Sehemu zote kwa Jiji zima kuwekwa Taa za kuongozea Magari na watembea kwa Miguu kwa Mkoa mzima wa Mbeya kiukweli hapa ndipo ambapo pamepewe kipao mbele hicho cha kuwekewa Taa za kuongozea Magari na Watembea kwa Miguu, Lakini cha kushangaza zaidi licha ya eneo hilo kupewe kipaombelele kumekuwa na Vijipu Upele vingi ambavyo vinajitokeza mara kwa mara katika eneo hilo ikiwemo hili la Taa moja Kupigwa Ngwala na Gari na kutelekezwa kama uionavyo hapo katika Taswira ikiwa na Mmoja wa watembea kwa Miguu akisubiri Taa hiyo iweze kumuongoza lakini hali ya kuwa Taa hiyo ikiwa hoi Bin Taabani kutokana na kupokea Ngwala na Gari ambayo hatukuweza Kuifahamu.
Kichwa cha Taa hiyo Mpya iliyo wekwa hivi karibuni kuajili ya kuongozea Wananchi watumiao Barabara hiyo ikiwa katika Uso wa simanzi Kando kando ya Eneo hilo la Mafiati Mataa Jijini Mbeya..
Mmoja kati ya watumiaji wa Barabara hiyo akisubiri Msaada wa Mbinu nyengine ya kumuwezesha kuvuka Barabara kutokana na kumsubiri Muongozaji wake alie Pigwa Ngwala bila mafanikio.
PICHA NA MR.PENGO MMG.
Post a Comment