Friday, March 4, 2016

UPENDO GOSPEL YAANDAA TAMASHA LA PASAKA LITAKALOFANYIKA MACH 27 VIWANJA VYA LEADER'S.

Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's akizungumza na waandishi wa habarin (hawapo pichani) juu ya tamasha la pasaka litakalofanyika Machi 27 katika viwanja vya leadar's jijini Dar es Salaam,katika ni Maneja Uendeshaji, Shaweji Steven, Kushoto ni Meneja wa Gospel, Emmanuel Mweta.
02.Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's wakati akitangaza tamasha la pasaka la Machi 27 mwaka huu leo jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
UPENDO Music Festival imeandaa tamasha la Injili litakalofanyika  Machi 27 mwaka huu katika viwanja vya Leader,s jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's amesema  kuwa tamasha hilo litakuwa  na ubora kutokana na walivyoliandaa kwa miaka mingi na sasa imetimia waumini mbalimbali kuungana kuikaribisha pasaka.

Charle's amesema kuwa tamasha litakuwa na vionjo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa injili katika wa vikundi mbalimbali bila kujali kanisa analotaka.

Amesema wamekuja katika tamasha kwa muonekano tofauti kwa wasanii kutumia majukwa tamasha hilo kujitangaza na sio kupigiwa simu hali hiyo ndio imesaidia nchi zilizoendelea kuwa na wasanii nyota kutokana na kujitoa katika matamasha.

Tamasha hilo litakuwa na viingilio ikiwa kama sehemu ya uendeshaji wa uwanja na sio kwa ajili ya kujinufaisha kwa kuwa na kiingilio kwa mkubwa sh.5,000 na viti maalum kwa sh.10,000.

Charle's amesema kuwa kuanzia majira saa nne kutakuwa na michezo mbalimbali katika viwanja hivyo nia ikiwa na kutambua na vipaji vingine vya michezo.

No comments: