Friday, March 4, 2016

ENEO LENYE VICHAKA KATIKA FUKWE ZA COCO LAANZA KUFYEKWA.

ENEO korofi la Oystarbay hadi ufukwe wa Coco ambalo lipo pembezoni mwa  bahari ya hindi  ambalo lilikua kificho cha waharifu limeanzwa kufanyiwa usafi kwa kufyekwa ili kupunguza uharifu kwa wapitanjia wa eneo hilo.

Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Mtaa wa Oystarbay, Zefrin Lubuva wakati akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa eneo hilo lilikuwa kificho cha waharifu ambao walikuwa wanapora baadhi ya wananchi wanao tumia eneo hilo.

Lubuva amesema kuwa pembezoni mwa eneo hilo wanaishi baadhi ya mabalozi wa nchi za Ubelgiji na kituo kidogo cha biashara cha ubalozi wa India ambapo ndipo walipoanzia kufanyia usafi kwa kufyeka vichaka vya maeneo hayo ambavyo vilikuwa vinaiziba bahari ya hidhi kuonekana kwa ulahisi kwa wakazi wa eneo hilo.

Pia amesema kuwa kwa sasa tangu kufyekwa kwa vichaka hivyo bahari ya hindi imekuwa ikionekana vizuri na kuonekana upande wa pili ambapo mwanzoni haikuwa hivyo. 

Kwa upande wa wakazi wa eneo hilo wamemshukuru Mwenyekiti wa Mtaa wa Oystarbay, Zefrin Lubuva kwa kuchukua uamzi mzuri kwa kufyeka eneo hilo kwani waharifu waliona kama makazi yao kwaajili ya kukwapulia wapitanjia vitu vyao. 
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Oystarbay Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika  sehemu iliyofyekwa ambayo ilikua sehemu hatarishi kwa raia wanaotumia eneo hilo lililopo  pembezoni mwa bahari ya hindi oysterbay hadi ufukwe wa coco.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Oystarbay Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akionyesha vichaka amavyo ni hatari kwa jamii kwani baadhi ya wananchi wameweka eneo hilo kama dampo la kutupa takataka na wengine wameweka eneo hilo kama maliwato ikiwa eneo ni la fukwe za bahari ya hindi.

 Eneo la lililokuwa na kichaka chenye miiba likionekana likiwa limefyekwa
, ikiwa eneo hilo linaendelea kufyekwa kwaajili ya kuweka eneo safi.
  Mhanga wa kuibiwa katika eneo la fukwe za coco jijini Dar es Salaam, Manfred Nyachi. amewashukuru uongozi wa mtaa wa Oysterbay kwa kuchukua uamuzi wa kufyeka vichaka hivyo kwani umekua ukitia hasara kwa wananchi ambao ni watumiaji wa eneo hilo kwani waharifu wanaowaibia watu katika maeneo hayo walikuwa wakikimbilia katika vichaka vya maeneo hayo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

No comments: