All Right Receved by MR.PENGO 2016

Tuesday, October 20, 2015

MEYA MANISPAA YA KINONDONI ANAYEMALIZA MUDA WAKE YUSUPH MWENDA AZINDUA UZIO WA KISASA SHULE YA MSINGI MIKOCHENI A NA KUWAAGA RASMI WANANCHI WA KATA HIYO....

 Meya wa Manispaa ya Kinondoni anayemaliza muda wake, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto) akifuatilia kwa makini matukio ya sherehe hizo sambamba na watendaji.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni anayemaliza muda wake, Yusuph Mwenda akicheza muziki na vijana wa kundi la muziki la Sholo Mwamba wakati wa sherehe za uzinduzi wa uzio wa kisasa wa  Shule ya Msingi Mikocheni A sambamba na kuwaaga rasmi wakazi wa Kata hiyo baada ya kumaliza kuwatumikia.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni anayemaliza muda wake, Yusuph Mwenda akiwahutubia wakazi wa Kata ya Mikocheni A wakati wa sherehe za uzinduzi wa uzio wa kisasa wa Shule ya Msingi Mikocheni A sambamba na kuwaaga wakazi hao, mwishoni mwa wiki.

  Vijana wa timu za Kata hiyo wakichuana katika bonanza la sherehe hizo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man akitumbuiza katika bonanza la sherehe hizo.
Mwimbaji wa nyimbo za mipasho, Isha Mashauzi akitumbuiza katika bonanza la sherehe za uzinduzi wa uzio wa kisasa wa Shule ya Msingi Mikocheni A, Manispaa ya Kinondoni mwishoni mwa wiki.
Post a Comment