All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, August 9, 2015

MSAADA TUTANI: SHILINGI MILIONI 50 ZINAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YA KIJANA HUYU..

Kijana ABEL MACHANG'A, mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa Jijini Dar es Salaam, ambae anasumbuliwa na maradhi ya macho, akiwa amejipumzisha nyumbani kwao baada ya kuzungumza na waandishi wa habari ili kuomba msaada wa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.  

Na Mwandishi Wetu

Kijana Abel mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam anakabiliwa na maradhi ya macho na mishipa ya fahamu hali iliyosababisha apoteze uwezo wa kuona, na hivyo kuhitaji msaada wa wasamaria wema ili apelekwe nchini India kwa matibabu zaidi.

Ama kweli kabla hujafa hujaumbika! Kijana ABEL MACHANG’A aliyezaliwa miaka 23 iliyopita alikuwa na uwezo wa kuona kama kawaida na alisoma mpaka kidato cha nne na baadaye kujiunga na elimu ya biashara katika chuo cha biashara cha CBE cha jijini Dar es Salaam.

Lakini hivi sasa kijana huyo haoni tena baada ya kupata maradhi ya macho yaliyosababisha macho yake kuvimba na kutoka nje licha ya kupatiwa matibabu.
Baba wa kijana huyo amesema jitihada za kutibiwa nchini zimeonekana kutokuwa na mafanikio na kuomba wasamaria wema na mashirika mbalimbali yajitokeze kumsaidia kijana huyu gharama za matibabu takribani milioni Hamsini.

Kwa yeyote atakayeguswa na maradhi ya kijana huyu, awasiliane na Chumba cha Habari Clouds Tv Mikocheni jijini Dar es Salaam au awasiliane na baba mzazi wa kijana huyo kwa namba 0713 275740 au 0784 275740.
Post a Comment