All Right Receved by MR.PENGO 2016

Tuesday, July 21, 2015

Wanafunzi wawili walipiwa ada kwa malipo ya bima ya mama yao...


Mratibu Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, akizungumza na baadhi ya watumishi wa shule ya sekondari James Sangu (hawapo pichani ) juu ya namna ya kujiunga na fao hilo kabla ya kufanyika kwa zoezi la makabidhiano ya hundi kwa Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mama yake Anna Jelle kufariki Dunia. Picha zote Emanuel Madafa, Mbeya.Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Financial Services, jana imewakabidhi wanafunzi wawili hundi ya Sh Milioni tatu, itakayowawezesha kila mwaka kupata Sh Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa ajili ya ada kwenye shule zao wanazosoma kutokana na malipo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao inayoendeshwa na taasisi hiyo.

Wanafunzi hao ni Jacqueline Ndyamkana wa shule ya sekondari ya James Sangu na Joceline Ndyamkana wa shule ya awali, huku malipo hayo yakitokana na bima ya mama yao aliyejulikana kwa jina la Anna Jelle, ambapo kwa kupewa kiasi hicho cha fedha kila mwaka, kutawafanya wasome bila usumbufu wowote katika kipindi hicho cha miaka mitatu mfululizo.
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura,akionyesha moja fomu maalumu zinazotumiwa na wateja wao katika hautua za awali wakati wa uombaji wa mkopo kupitia taasisi hiyo.
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, akitoa ufafanuzi kuhusiana changamoto mbalimbali zinazowakibili wateja wao na namna ambavyo walivyo weza kuhudumia wateja wao.

Alpha Akimu Meneja wa Kanda za Nyanda za juu Kusini akizungumza katika hafla hiyo.
Akizungumza jana wilayani Mbozi, mkoani Mbeya, Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Financial Sercices, Ruth Bura, alisema kwamba fedha hizo zinatoka kwa ajili ya kuwezesha watoto hao wawili.

Baadhi ya walimu wa shule ya Sekondari James Sangu iliyopo Vwawa, Mbozi mkoani Mbeya, wakiuliza maswali kwa Mratibu wa
Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, (hayupo pichani) juu ya huduma zinazotolewa na Taasisis hiyo.
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, kushoto akimkabidhi rasmi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3,000,000, Jacqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Jamsi Sangu iliyopo Vwawa Mbozi ambaye alifiwa na mzazi wake ambaye alikuwa mteja wa Bayport.

Shughuli ikiendelea
Watu wakiuliza maswali
Makabidhiano yakiendelea
Makabidhiano ya hundi yakiendelea
Makabidhiano yakiendelea
Picha ya pamoja
Asante kwa hundi
Alisema taasisi yao iliamua kuanzisha huduma hiyo ya bima ya elimu kwa uwapendao ili kuhakikisha kwamba watoto wanaendelea kupata elimu zao, hata inapotokea wazazi wao wanafariki Dunia.“Ndugu yetu Anna Jelle alijiunga na huduma yao Aprili 14 mwaka jana, ambapo mwaka huu ilitokea bahati mbaya akafariki Dunia, hivyo tukaona tuwape watoto hawa stahiki zao ili waendelee na masomo yao.

“Watoto hawa watapata Sh Milioni moja kwa kila mwaka na watapewa fedha hizi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, tukiamini kuwa tunaweza kurahisha masomo yao japo kwa kipindi hiki ambacho mzazi wao hayupo,” alisema. Naye Jacqualine aliishukuru Bayport kwa kuanzisha huduma hiyo muhimu, akiamini kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo anaweza kuwa katika mazingira mazuri kwenye masomo yake na mdogo wake.

Kwa mujibu wa Ruth, malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu, huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000 na makato ya bima ya Silver ni Sh 7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000 wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi na kusisitiza kwamba ambapo mbali na bima, taasisi yao pia inatoa huduma ya mikopo ya bidhaa bila kusahau mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Post a Comment