Monday, June 15, 2015

DAWA ZA KUZUIA KUYUMBA KWA NDOA ZAWEKWA WAZI.....

 Baadhi ya wataalamu wa Kiislam wakimsilizi kwa Makini Dr Ahmad Totonji Kutoka Suadi Arabia alipokuwa akiwakilisha Mada ya Taasisi ya Ndoa, Jana, leo na Kesho Katika Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Dr. Totonji  amewasihi waislam wataalamu kuwa chachu ya mfano wa Ndoa Imara katika Jamii.
  Dr. Ahmed Totonji (Mwenye Kanzu) akiteta Jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Banki Dr. Muhsin Muhsin wakati wa Kongamano la wataalamu wa Kiislam la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotegemewa kuanza katikati ya wiki hii.
 Mh. Asha Mtwangi akichangia Mawazo juu ya Kauli Mbiu ya Kongamano la Kukaribisha Mwezi wa Ramadhan ambayo ilikuwa Ndoa Chanzo Cha Utu wetu ambalo mada ya Taasisi ya Ndoa: Jana, Leo na Kesho pamoja na Familia katika Changamoto ya utandawazi. Mh. Asha Mtwangi alihamasisha taasisi mbali mbali kuweka nguvu zaidi kuwapa mafunzo ya dini vijana na wanandoa ili kuhakikisha wanafahamu majukumu sahihi ndani ya ndoa.
 Wajumbe wa Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wakimsikiliza Muhubiri wa Kimataifa Dr. Ahmed Totonji kutoka Saudi Arabia alipokuwa akitoa mada yake na kuwapa Changamoto waislam na dunia juu ya Umuhimu wa kurudi katika malengo sahihi ya Muumba wao kama tunahitaji maendeleo sahihi ya Utu wa Binaadamu.
 Dada Sadaka Gandi akiwakilisha mada ya Familia katika Changamoto za utandawazi ambapo aliitaka jamii hasa waislam kuwa karibu na familia zao na watoto wao kama wataka hasa kupambana hatari kubwa za utandawazi ambao upo Mitaani, Mashuleni pamoja na katika Simu za Mkononi.

No comments: