All Right Receved by MR.PENGO 2016

Tuesday, May 12, 2015

WAZIRI MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI TANROADS-MOROGORO.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa ameshikana mikono na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara, TANROADS Eng. Patrick Mfugale kushoto pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe kulia wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mkoani Morogoro. Waziri Magufuli amewapongeza TANROADS kwa utendaji kazi wao mzuri ujenzi wa Barabara nchini.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma risala kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli.TANROADS imepata TUZO ya mfanyakazi bora na mwajiri bora kutoka TAMICO.
Baadhi ya Wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia tuzo aliyokabidhiwa na Wafanyakazi wa TANROADS kwa kutambua uongozi wake bora katika kuanzisha na kule Wakala huo tangu mwaka 2000-2015.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mara baada ya mkutano uliofanyika mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mkoani Morogoro. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.SOMA ZAIDI HAPA.
Post a Comment