All Right Receved by MR.PENGO 2016

Monday, May 25, 2015

UNESCO YASISITIZA UPENDO KWA WATOTO WENYE ALBINISM.

DSC_1025
 hii ndio hali halisi ya binti huyu katika mikono yake kutokana na kutembea kwenye jua bila kusitiri mikono yake na nguo ndefu.
DSC_0945
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akiambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (kushoto) walipotembelea shule msingi Mitindo ya watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza. Kulia ni Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO Tanzania, Bi. Annica Moore.
Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Modewjiblog team
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)Tanzania, Zulmira Rodrigues amesisitiza umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ulemavu wa ngozi katika jamii baadala ya kuwatenga .
Zulmira alisema hayo alipotembelea watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi ya Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza mwishoni mwa juma
Shule hiyo ya serikali ina wanafunzi zaidi ya 1000 wakimo wenye ulemavu 202 .
Kati yao 81 ni wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ambao wanahifadhiwa na serikali katika shule hiyo maasa 24 kufuatia wimbi la mauaji la watu wenye ulemavu wa ngozi katika mikoa ya kanda ya ziwa .
Hata hivyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO Tanzania alionekana kupatwa huzuni kubwa kutokana hali ya maisha ya watoto hao .
“ Nimehuzunika sana (I am so sad). Sio tabia ya watu wa Afrika kuwatenga watu wanyonge (weak people)”alisema huku akitokwa na machozi mara baada ya kuwatembelea watoto hao na kuongea nao pamoja na uongozi wa shule hiyo.
Alisema ni muhimu watoto hao wenye ulemavu wa ngozi kuwa wanavaa nguo za mikono mirefu ili kuwakinga na jua kwa ajili ya kulinda afya zao.
Hata hivyo Zulmira alipongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi na kutoa wito kwa wadau wote kuunga mkono juhudi hizo.
DSC_0955
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwalimu msingi Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Katika ziara hiyo, Zulmira alikuwa amefuatana na mbunge wa viti maalum anayewakilisha watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) Mh. Al shaymaa Kwegyir.
Mbunge huyo pia alisema kitendo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kukosa malezi na mapenzi ya wazazi ni changomoto kubwa iliyopo kwa sasa.
Alisema ni jukumu la watu wote kulinda na kusadia kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
“Ufumbuzi wa matatizo ya wetu wenye ulemavu wa ngozi sio kazi ya serikali tu, ni jukumu la kila mtu”,mbunge huyo alisisitiza.
Aliahidi kuwasilisha bungeni baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi walemavu waliopo katika shule hiyo ya Mitindo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kurwa Ng’hwelo alisema serikali inatumia zaidi ya shilingi milioni 10 kuwa ajili ya mahitaji ya chakula kwa wanafunzi wote wenye ulemavu wapatao 202 kila mwezi.
Shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wanaosadia wanafunzi hao walemavu.
DSC_0968
Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo akitoa maelezo ya idadi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shuleni hapo ambao ni 202 huku 81 wakiwa na albinism kwa Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyetembelea shule hiyo kuangali changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0979
Mwalimu wa shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo akimwonyesha mazingira ya eneo la shule hiyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues aliyeambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
DSC_0989
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa kutwa wanaosoma katika shule ya msingi Mitindo mara baada ya kuwasili shuleni hapo akiwa ameambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir.
DSC_0993
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza na wanafunzi hao waliofurahia ujio wake.
DSC_0997
Pichani ni moja ya jengo lililojengwa na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
DSC_1009
Mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) akitoka bwenini kuelekea chumba maalum kwa ajili ya kujipatia chakula cha mchana katika shule ya msingi Mitindo huku akionekana kutembea kwenye jua kali pasipo na kuwa na nguo ndefu ya kufunika hadi mikononi kujikinga na mionzi ya jua inayopelekea kupata saratani ya ngozi.
DSC_1017
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albinism) ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akila chakula cha machana huku akijikuna kutokana na maumivu makali anayosikia ya majeraha ya mionzi ya jua iliyoharibu mikono yake na kubadilika rangi ambayo athari yake baadae ni saratani ya ngozi.
DSC_1026
Baadhi ya watoto wa bweni wenye Albinism wakijipatia chakula cha mchana jikoni.
DSC_1043
Mtoto mwingine aliyeathiriwa na mionzi ya jua miguuni na kupelekea kubadilika rangi kuwa mwekundu kutokana na kukosa nguo ndefu za kujisitiri na mionzi ya jua... wakiendelea kujinoma na chakula cha mchana.
DSC_1033
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akionyesha uso wenye huzuni kubwa kutokana na mazingira magumu waliyonayo watoto hao shuleni hapo. Kushoto ni Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir aliyeambatana na Bi. Zulmira Rodrigues kutembelea shule hiyo. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mitindo, Kulwa Ng'hwelo.
DSC_1068
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mitindo, Kalunde Cosmas alipofanya ziara fupi ya kutembelea shule hiyo na kujionea changamoto zinazowakibili watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism).
DSC_1036
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akimwonyesha mwandishi wa modewji blog (hayupo pichani) majeraha ya kuungua na jua kwa mmoja wa watoto mwenye albinism shuleni hapo.
DSC_1053
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyekuwa akijipatia chakula cha mchana.
DSC_1073
Mdau Semeni Kingaru akimsimamia kula chakula cha mchana mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism aliyeonekana kukosa upendo wa wazazi wake kwa kipindi kirefu na kufarijiwa na ugeni huo uliofika shuleni hapo.
DSC_1101
Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akibadilishana mawazo na mabinti wa shule ya msingi Mitindo alipowatembelea na Bi. Zulmira Rodrigues.
DSC_1106
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisaidiana na Mdau Semeni Kingaru kugawa zawadi ya juisi kwa watoto wa shule ya msingi Mitindo.
DSC_1113
Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO, Bi. Annica Moore aliyeambatana na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (hayupo pichani) akifurahi jambo wakati akigawa zawadi ya juisi mmoja watoto wenye albinism shuleni hapo.
DSC_1119
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendelea na zoezi la ugwaji zawadi ya juisi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio wa shule ya msingi Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza alipowatembelea mwishoni mwa juma akiwa ameambata na Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (hayupo pichani).
DSC_1085
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa macho wakijumuika na wenzao wenye ulemavu wa ngozi na masikio kujipatia chakula cha mchana.
DSC_1087
Mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism anayeonekana kukosa lishe bora inayostahili kutokana na umri wake ambapo modewjiblogimebaini kuwa mtoto huyu ana "Utapiamlo" kutokana na kukosa lishe hiyo bora. Dalili moja wapo ni tumbo lake kuwa kubwa na gumu.
DSC_1137
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnywesha juisi mtoto mdogo kuliko wote anayelelewa kwenye shule ya msingi Mitindo ya watoto wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu wa ngozi, macho na masikio alipofanyia ziara fupi mwishoni mwa juma mkoani Mwanza.
DSC_1144
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimnyeshwa juisi mtoto menye ulemavu wa macho alipotembelea shule ya msingi Mitindo iliyopo wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza.
DSC_1160
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa na uso wa huzuni kutokana na mazingira ya watoto hao na kupelekea kumwaga machozi kwa uchungu yeye kama mama mwenye kuthamini upendo. Kushoto ni Mh. Al Shaymaa Kwegyir.
DSC_1163
Bw. Abdulaziz Mbegele wa kitengo cha Logistic kutoka UNESCO, akimnywesha juisi mtoto mwenye ulemavu wa macho wakati wa ziara hiyo na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania.
DSC_1091
Mtoto alyefahamika kwa jina moja tu Kevin mwenye umri wa miaka 11 ambaye alifikishwa kwenye shule hiyo akiwa mdogo sana na wazazi wake kumtelekeza hadi leo huku akiwa hamjui mama, baba, mjomba, dada, kaka wala shangazi..... kisa amezaliwa na albinism....!
DSC_1097
Mtoto Kevin akipata "self" na mjomba wake mpya Zainul Mzige wamodewjiblog aliyeambatana na ugeni huo.
DSC_1202
Mkuu wa ofisi na Mwakililishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na waandishi wa habari na kutoa hisia zake kuhusiana na changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu wa nguvu na kusisitiza upendo kwa watu wenye albinism.
DSC_1195
DSC_1216
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Post a Comment