Wednesday, April 15, 2015

WALIOFARIKI KWA RADI MKOANI KIGOMA WAAGWA KWA MAZISHI MCHANA HUU.

  Miili ya Wanafunzi sita na Mwalimu ikiwa tayari kwa kuagwa katika viwanja vya shule ya Msingi Kibirizi mkoani Kigoma .  WATU wanane wakiwemo wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi kibirizi mmoja pamoja na mtu wa kawaida mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapo  walipoteza maisha hapo jana baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengine 15 kujeruhiwa na radi hiyo.

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya akisoma salamu za rambi rambi za mkoa wakati wa kuaga miili ya Wanafunzi na Waalimu waliopigwa na radi jana.
 Katibu wa Bakwata mkoa wa Kigoma,Shekhe Moshi Guoguo akituma salamu za rambirambi kwa wafiwa.
 Wanajeshi wa JWTZ wakiingiza miili ya marehemu katika viwanja vya shule ya msingi Kibirizi kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

No comments: