Sunday, April 12, 2015

TATIZO LA RUSHWA YA NGONO BADO NI TATIZO TANZANIA.

Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini tanzania mama EUSEBIA MUNUO  ambaye alikuwa ndiye mkufunzi katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa leo jijini Dar es salaam
 Rushwa ya ngono pamoja na matumizi mabaya ya madaraka yametajwa kuwa ni moja kati ya matatizo makubwa ambayo yamezidi kuweka mizizi nchini tanzania na kuwaadhiri wasichana wengi huku sheria ikishindwa kuweka wazi adhabu mahususi ili kuwabana wanaohusika katika swala hilo.
Wanafunzi mbalimbali kutoka chuo kikuu Dar es salaam waliohudhuria katika mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa tatizo la ruswa ya ngono limekuwa likiongezeka siku hadi siku nchini kutokana na kutokuwa na sheria mahususi ambayo inawaadhiu moja kwa moja  wahusika katika swala hilo.
  
Amesema kuwa wasichana wengi wanapokuwa katika harakati za kutafuta ajira katika maofisi mbalimbali wamejikuta wakitumia miili yao kuwashawishi mabosi wao ili waweze kupata ajira jambo ambalo amesema kuwa sio sahihi na wasichana hao wamekuwa wakikosa msaada kuhusu swala hilo.

  Amesema kuwa hata katika maofisi mbalimbali kumekuwa na wasichana ambao hawana vigezi vya kuwa katika maofisi hayo ila wapo tu kwa sababu wanatembea na mabisi wao jambo ambalo limetajwa kuleta madhara makubwa ikiwemo kushusha ufanisi wa kazi pamoja na ofisi husika kwa ujumla.
Mwanafunzi CATHERIN OLOMY akizungumza na mwandishi wa mtandao huu juu ya mafanikio ya semina hiyo ya siku moja kwao na kwa jamii kwa ujumla
Baadhi ya wanafunzi ambao wamehuduria mafunzo hayo ya siku moja ambayo yameandaliwa na WILAK kwa kushirikiana na TAWLA mwanafuzni CATHERINE OLIMY ambaye ni mmoja ya washiriki anasema kuwa  mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wanafunzi wa sasa hususani wasichana kwa kuwa yatawasaidia kujiamini kujua haki zao kama wanafunzi na watoto wa kike,ikiwa ni pamoja na kujua udhamani wao pindi wanapokutana na swala la rushwa ya ngono.

No comments: