All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, April 19, 2015

ORIGINAL KOMEDI WAZURU PSPF, LENGO NI KUJIONEA UBORA WA HUDUMA ZA MFUKO HUO.

Wasanii wanaounda kundi la Original Komedi wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Lonick Nkinda, Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko huo, wasanii hao walitembelea Makao Makuu ya PSPF ili kujionea utendaji wa Mfuko huo.
Msanii wa kikundi cha Original Komedi Bw. Emmanuel Mgaya akijaribu kufungua moja ya mitambo inayotumika kuhifadhia kumbukumbu za wanachama wa PSPF ili kuona ubora wa huduma za Mfuko huo.
Wasanii wa kundi la Original Komedi wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF pamoja na watendaji wengine wa Mfuko huo baada ya kufanya ziara ya siku moja kujionea utendaji wa Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa wasanii wa kundi la Original Komedi baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mfuko, pichani wasanii hao wakiwa katika jengo jipya la PSPF lililopo katika Barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu (kulia) akiongea wasanii wa kikundi cha Original Komedi walipotembelea Makao Makuu ya PSPF kwa ajili ya kujionea ubora wa huduma zinazotolewa na Mfuko huo.
Post a Comment