All Right Receved by MR.PENGO 2016

Wednesday, February 25, 2015

WATANZANIA WAASWA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NDANI YA NCHI.NA FRANK KIBIKI, IRINGA
SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limewataka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani, badala ya zile zinazoingizwa kutoka nje ili kukuza uchumi wan chi.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya alisema ikiwa watanzania wataenzi bidhaa zinazotengenezwa ndani itakuwa rahisi kuinua uchumi wa nchi, na mtu mmoja mmoja.


Alisema shirika hilo limekuwa likitengeneza bidhaa nyingi, zikiwemo mashine na pembejeo za kilimo lakini, kutokana na dhana ya kununua bidhaa za nje wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la soko.


“Tunazalisha mashine mbalimbali, zikiwemo zana za kilimo kama vile, mashine za kusagia nafaka, kuchujia mafuta ya alizeti, kukamulia asali na nyingine nyingi lakini changamoto kubwa ni soko la bidhaa za ndani,”alisema.


Aidha alisema itakuwa vyema kama serikali itaweka utaratibu au sera itakayofanya watu wajenge tabia ya kuheshimu, kupenda na  kutumia bidhaa za ndani.


Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali na wakulima walisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakinunua mashine za kichina kutokana na bei yake kuwa chini ingawa hazina ubora.


“Bidhaa za nje ni bei ndogo kuliko zile zinazotengenezwa ndani, hii ndiyo sababu inayofanya wengi tutumie bidhaa za kichina ambazo hata hivyo hazidumu kwa muda mrefu,”alisema LeoniKA Sanga, mmilikiwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, mjini Iringa.


Aliiomba serikali kutoa ruzuku kwa SIDO ili bidhaa zinazotengenezwa zishushwe bei yake na kuweza kuwahudumia wajasiriamali na wakulima wadogo.
KAIMU MENEJA WA SIDO MKOA WA IRINGA, MR NIKO MAHINYA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFINI KWAKE
KAIMU MENEJA WA SIDO MKOANI IRINGA, NIKO MAHINYA AKIWA NA MHANDISI WA KARAKANA YA SIDO IRINGA, MICHAEL MATONYA WAKATI WAKITEMBELEA UTENDAJI KAZI WA KARAKANA HIYO
FUNDI WA KARAKANA YA SIDO ELAYSON TARIMO AKIANGALIA MASHINE YA KUNOA VYUMA, AMBAYO ILIKUWA IKINOA MAJEMBE YA KUKATIA CHAI
MSIMAMIZI WA KARAKANA YA KUTENGENEZEA MASHINE MBALIMBALI YA SIDO MKOANI IRINGA, LEONARD LUMATO AKIENDELEA NA KAZI KATIKA KARAKANA HIYO

KIJANA AKIENDELEA NA KAZI NDANI YA KARAKANA
Post a Comment