Meneja
wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Mkoani Kusini Pemba, Bw. Ali
Abbas akisoma risala ya kituo chake mbele ya mgeni rasmi Waziri wa
Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto visiwani
Zanzibar, Mh. Zainabu Omari Mohammed (hayupo pichani) wakati wa sherehe
za uzinduzi wa kituo hicho cha redio.
Mabinti
wa visiwani Pemba wakisoma utenzi wa kulishukuru shirika la UNESCO na
ZBC kwa kuanzisha kituo hicho cha Redio jamii jimbo la Mkanyageni mkoani
Kusini Pemba.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani
Zanzibar, Juma Yakufi akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri mwenye dhamani
ya wizara hiyo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo
la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki
visiwani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba, Hemedi Selemani akitoa neno la
shukrani wakazi wa mkoani jimbo la Mkanyageni pamoja na wageni waalikwa
kwenye sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba
uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza kwenye uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba
uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akimkabidhi cheti Meneja wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Ali
Abbas wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio jamii hiyo.
Meza kuu.
Mkuu
wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba, Bi. Mwanajuma
Abdallah akizungumza machache na wakazi wa mkoani na kuwaasa kukitumia
chombo hicho vyema katika kujiletea maendeleo na kupashana habari kabla
ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua rasmi kituo hicho cha Redio Jamii.
Waziri
wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab
Omar Mohammed akisoma hotuba yake kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo
cha redio ya jamii jimbo la Mkanyageni, Mkoani Kusini Pemba.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wakazi wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini
Pemba wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi kwenye sherehe za
ufunguzi wa kituo hicho cha Redio Jamii.
Pichani
juu na chini ni Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake
na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akikabidhi vyeti kwa baadhi ya
wafanyakazi wa Redio Jamii Mkoani ya jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini
Pemba. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja
wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani Zanzibar, Juma Yakufi.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto,
Mh. Zainab Omar Mohammed akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
kituo cha Redio Jamii Mkoani iliyopo Kusini Pemba. Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba, Bi.
Mwanajuma Abdallah (mwenye mtandio wa bluu), Mkuu wa Wilaya ya Mkoani
Kusini Pemba, Hemedi Selemani pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Sasa kimezinduliwa rasmi....!
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto,
Mh. Zainab Omar Mohammed akitia saini kitabu cha wageni cha kituo cha
Redio Jamii Mkoani Kusini Pemba kabla ya kukagua vifaa na studio ya
kituo hicho.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto,
Mh. Zainab Omar Mohammed akizungumza Live na wananchi wa jimbo la
Mkanyageni mkoani Kusini Pemba mara baada ya kuzindua kituo cha Redio
Jamii Mkoani ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za Mapinduzi mwishoni
mwa wiki kisiwani Pemba. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na washika dau kutoka UNESCO.
Mtangazaji
wa kituo cha Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Seif Mohammed
akiwa kwenye mahojiano na Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa
jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed yaliyorushwa
Live na kituo hicho mara baada ya kuzinduliwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto,
Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Redio
Jamii Mkoani, Wajumbe wa Bodi ya Redio Jamii Mkoani, wafadhili pamoja
na baadhi ya wageni waalikwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto,
Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya
Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba.
Mshauri
na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha na wanafunzi
wake wa vituo vya redio jamii ya Mkoani na Micheweni mara baada ya
sherehe za uzinduzi.
Kikundi
cha Ngoma ya Msembwe cha kisiwani Pemba kikitoa burudani kwenye
uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani uliofanyika mwishoni mwa juma Kusini
Pemba.
No comments:
Post a Comment