Sunday, January 4, 2015

DORIS MOLLEL ACHANGIA WATOTO WALIO ZALIWA KABLA YA MUDA WA KAWAIDA (NJITI) KATIKA HOSPITALI YA MKOA SINGIDA.

Redds Miss central Zone 2014/15 Doris Mollel akisaini kitabu cha wageni katika hospitali ya mkoa Singida kabla ya halfla ya kukabidhi mashine mbili za kupumulia kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wa kawaida zenye thamani ya Tsh milioni 1.2. Waliopo nyuma ni warembo wengine wa Redds Miss Central Zone Linda Bureta, Blath Chambia na Suzy Wahere.
Doris Mollel akisema Maneno machache wakati akikabidi mashine mbili za watoto kupumulia zenye thamani ya Tsh millioni 1.2 kwa hospitali ya mkoa wa Singida kwa ushirikiano na Manifester brand.
Doris akikabidhi mashine 2 za msaada wa watoto kupumulia zenye thamani ya Tsh milioni 1.2 kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Daniel Tarimo, msaada kwa ushirikiano na Manifester brand. Mgeni rasmi kwenye hafla hii alikua ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi (hayupo pichani).
Makabidhiano. Mashine mbili za msaada wa watoto kupumulia zilitolewa kwa ushirikiano na Manifester brand.
Doris katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi, Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Daniel Tarimo, Muandaaji wa Miss Singida Bi. Bora Lemmy na warembo wengine wa Redds miss Central Zone.
Doris kwenye picha ya pamoja na warembo wenzake wa central zone walioenda kumuunga mkono. Linda Bureta, Blath Chambia na Suzy Wahere.
Akiwa na wafanyakazi wa wodi ya watoto
Alipata nafasi ya kuwaona watoto hawa wawili wazuri kwenye wodi yao
Kwenye picha nyingine ya pamoja.
Mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wa kawaida akiwa kwenye mrija wa kumsadia kupumua uliounganishwa na mashine kama ambazo zimekabidhiwa na Doris.
Alipata nafasi ya kuwasimulia baadhi ya kina mama waliojifungua watoto njiti kuhusu historia yake na kuwapa moyo kwamba hata watoto wao pia watakua na kufanikiwa kufika popote pamoja na kuzaliwa njiti.
Wakiwa na nyuso za furaha

No comments: