Monday, January 19, 2015

MBUNGE JAMESN MBATIA AWASHUKURU WANANCHI JIMBO LA VUNJO KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ghalani katika mji mdogo wa Himo jimbo a Vunjo alipokuwa akiwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kukipa ushindi chama chake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa ulimalizika hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza na wananchi katika jimbo la Vunjo,wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuwashukuru kwa kuchagua wenyeviti wengi waliotokana na chama cha NCCR-Mageuzi,mkutano uliohutubiwa pia na Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.
Mh Nassari na Mh Mbatia wakitoa salamu kwa mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo . Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,(Chadema) jimbo la Vunjo wakiteta jambo wakati wa mkutano wa hadhara  uliofanyika katika viwanja vya Ghalani ,mji mdogo wa Himo ,mkutano uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Vunjo kukipa chama hicho viti vingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji. Baaadhi ya viongozi waliochaguliwa wakati wa uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Mamia ya wananchama na mashabiki wa chama cha NCCR-Mageuzi wakimsikiliza ,Mh Mbatia(hayupo pichani)
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: