Wednesday, January 7, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AWATEMBELEA NA KUWAFARIJI WAZEE WAASISI WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji mke na mtoto wa marehemu Mzee Makame Shekha aliyekua muasisi wa TANU na ASP, alipofika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Moga Mpitile Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Januari 07,2015 kwa ajili ya kufariji na kutoa pole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Machano Mjombo (102) mmoja kati ya Waasisi wa TANU na ASP wakati alipomtembelea kijijini kwake Gamba Mabatini Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kumjulia hali leo Januari 07,2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafamilia ya marehemu Mzee MtumwaKassim, wakati alipowatembelea kijijini kwao Gamba Sokoni Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kuwafariji leo Januari 07,2015. (Picha na OMR)

No comments: