Wednesday, January 14, 2015

FLAVIANA MATATA FOUNDATION YATOA VIFAA VYA SHULE SHULE YA MSINGI MSINUNE.

flaviana matata 2015Taasis ya Flaviana Matata 'FMF' ya Mwanamitindo Flaviana Matata aishie New York ,Nchini Marekani. Mwaka jana ilisaidia watoto 3000 kwa kuwapa vifaa vya kujifunzia.Mwaka huu itaendelea kuwasaidia Watoto hao hao wakati inaangalia namna ya kutatua matatizo mengine yanayozikabili Shule hizo ili kuboresha elimu nchini Yakiwemo mavazi, majengo na hata vyakula vya shule kwa shule za pembezoni Zoezi litaendelea kwa shule zingine za mikoani ukiwemo Mkoa wa Shinyanga, Lindi na Arusha kwa kuanzia. Bado Flaviana Matata Foundation inahamasisha yeyote akataeguswa ikiwa ni shirika , kampuni au mtu binafsi atakaeguswa kuwasiliana nao kupitia info@flavianamatatafoundation.org au piga simu +255 784 200 680 .
IMG_6600
IMG_6607
Pichani ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo kata ya Kiwangwa katika wilaya ya Bagamoyo leo team ya FMF ilopotembelea Shule hiyo kuendelea zoezi lake.
IMG_6594 Msimu wa wanafunzi kurejea mashuleni ndio kwanza umeanza ukiwa kama kampuni, mtu binafsi ukiguswa na ungependa kusaidia tafadhali wasiliana na info@flavianamatatafoundation.org au piga simu +255 784 200 680

No comments: