Thursday, December 18, 2014

PROF-TIBAIJUKA SIWEZI KUJIUZULU KWA FEDHA YA TEGETA ESCROW.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi profesa Anna Tibaijuka amesema hawezi kijiuzulu katika nafasi ya uwaziri kutokana na fedha ya Tegeta ESCROW.

    Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa hayati Regency, Anna alisema udalali wake katika fedha hiyo ni kuuajili ya wanafunzi wa taasisi ya Johannson Girls Education trust.

 Alisema pesa hizo alizo zipata ni bil.1.66 ambazo zilitoka katika kampuni ya James Rugemalira ni kuuajili ya msaada wa shule za taasisi ya Johannson Girls Education Trust.

Alisema fedha hizo kuuingia katika akaunti yake ni kutokana na masharti kutoka kwa mtoa msaada ndugu James Rugemalira ambae alitaka fedha hizo ziingie katika akaunti ya benk ya Mkombozi."Nikijihuzulu ata raisi Jakaya Kikwete atanishangaa, kwani zile fedha ni kuajili ya kukuza Elimu yetu nchini"

 waziri wa Ardhi, nyumba na makazi Prof-Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari juu ya fedha ya Tegeta Escrow.katika ukumbi wa hayyat Regency jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari walio hudhuria kikao hicho kilicho itishwa na waziri wa Ardhi, nyumba na Makazi Prof-Anna Tibaijuka.

No comments: