Tuesday, December 16, 2014

BAADHI YA MAENEO JIJINI MBEYA YAKITHILI KWA UCHAFU.

Hili jambo si mara ya kwanza kutokea jijini humo,ziara fupi ilio fanywa na kameramani wetu wa libeneke hili  jijini humo,katika kusahihisha mitaa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha mambo kitaani ni shwari,lakini imekua tofauti katika baadhi ya mitaa kwa kero ya kukithiri kwa uchafuzi wa mazingira.
 ni hali ya kusikitisha kwa kweli hii hali ni tete inahatalisha maisha ya wengi,jamani kweli hili swala sio la kulifumbia macho wakina bwana nanii tujitahidi kuzama mitaani na kushughulikia izi mambo jamani,hata wale tulio pita kwenye chaguzi za serikali za mitaa humu ndo kwa kuanzia sasa.
 hapa ni njiani na watu wengi hutumia njia hii kwa safari za hapa na pale napo hali si shwari.
 biashara zikiendelea huku nyuma kuna ghuba la kuhifadhia taka,lakini mama huyu hajari hilo kinacho angaliwa hapa ni mkwanja tuu.

                mitaro hii  imegeuzwa kama sehemu ya kuhifadhia taka.

 kama kawaida ya watoto nao wamo katika harakati za kuchagua chagua vifaa vya michezo katika sehemu hizo zilizo kithili kwa uchafuu.
               kuna mdau hapa katelekeza mazagazaga kando kando ya barabara.
madogo nao wakiendelea na udobi wa ku sop sop mifuko ya rambo kwa lengo la kuingia mzigoni,lakini maji yanayo tumika hapo mhh,kwaleo tuishie hapo endelea kufuatilia libeneke hili kila siku ujue kilicho jiri kitaani kwako.picha na Fadhiri Atick mr pengo.

No comments: