Safari hii iliandaliwa na Asasi mbili za Uyole Cultural Tourism Enterprises na ELIMISHA kwa ushirikiano na Chama cha waendesha baiskeli Mkoa wa Mbeya na Afisa Utamaduni wa Mkoa Bw.George Mbijima.
Awali, akiongea na wapenzi wa mchezo wa baiskeli,viongozi wa serikali na wanahabari
Awali, akiongea na wapenzi wa mchezo wa baiskeli,viongozi wa serikali na wanahabari
Awali, wakati wa kuwaaga waendesha baiskeli Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Elias Mwasandele amewashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kuwaunga mkono zaidi sana Uyole Cultural Tourism na ELIMISHA kwa kufanikisha jambo hilo.
Aidha,kwa kushirikiana na mhazini wake wa mkoa Bw.Lucas Mhagama wameutanabaisha umma kujiunga na mchezo huo kwani ni mzuri na una maslahi mazuri kwa mchezaji na Taifa kwa ujumla.
"....kama Mkoa wa Mbeya tumebahatika kupata mwaliko wa kupeleka wachezaji wanne kwenye mashindano ya baiskeli yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika ya Kusini...."Bw.Mwasandele alisikika akisema.
Baada ya kupata baraka zote za mkoa kutoka kwa Afisa Utamaduni Bw.George Mbijima aliyewaasa wachezaji kuimarisha umoja,upendo na mshikamano muda wote wa safari.
Waendesha baiskeli wafuatao walisafiri kutoka Mbeya Mjini hadi Wilayani Chunya umbali wa Kilomita 70, Tumejumuisha na muda waliotumia kufika:
1.Ipyana Mbogela-Saa 2:15
2.Elias Zawadi-Saa 2:17
3.Diego Fumbo-Saa 2:28
4.Moses Mwadonde-Saa 2:34
5.Daudi Selemani-Saa 2:56
6.Kianji Samson-Saa 2:59
Hata hivyo wachezaji wawili walishindwa kumaliza safari hiyo kutokana na matatizo yaliyojitokeza kwa baiskeli zao kupata pancha wakiwa wamebakiza Kilomita 10 kumaliza safari nao ni Kristola Senga na Pasia Tanganyika.
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mbeya Bw.George Mbijima (wa katikati aliyevaa tracksuit ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na waendesha baiskeli pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Uyole Cultural Tourism Enterprises na Elimisha kabla ya safari ya kuelekea Chunya
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mbeya Bw.George Mbijima akizungumza na waendesha baiskeli,viongozi na wananchi katika eneo la Rift Valley wakati akiwaaga waendesha baiskeli
Waendesha baiskeli wakiingia Wilayani Chunya baada ya kumaliza Kilomita 70 kutokea Mbeya Mjini.
No comments:
Post a Comment