Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios (kulia), akigongesha soda ya Coca-Cola na viongozi wengine wa kampuni hiyo kuashiria uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji hicho mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha (kutoka kushoto) ni David Karamagi - Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Nalaka Hettiaratchchi – Mkurugenzi wa Mauzo wa Coca-Cola Kwanza na Gary Pay – Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza Mbeya. Sambamba na uzinduzi wa muonekano mpya, Kampuni ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa zake mkoani Mbeya ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia teknolojia ya kisasa katika kiwanda chake kilichopo Mbeya. Picha zote na Mr. Pengo - MMG-MBEYA.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios, alisema upanuzi na kufunga mitambo ya kisasa zaidi katika kiwanda cha Coca-Cola mkoani Mbeya umefanyika wakati muafaka ambapo umeenda sambamba na mkakati wa kujiiimarisha zaidi katika soko la Mkoa huo na maeneo yote ya Nyanda za Juu Kusini na kuhakikisha bidhaa zake zinapatikana kila mahali na wakati wowote lengo likiwa ni kuwawezesha wakazi wa Mbeya kufurahia ladha murua ya kinywaji cha Coca-Cola na bidhaa nyingine zinazozalishwa na kampuni.
“Kampuni ya Coca- Cola inayo historia ya kuwepo mkoani hapa kwa muda mrefu, na tumeona ni vyema tukawashirikisha katika mkakati wetu wa mafanikio wenye lengo la kuongeza tija na ufanisi, ambapo tumeboresha kiwanda chetu na pia tumejipanga kusambaza bidhaa zetu kuhakikisha zinawafikia wananchi kwa urahisi na mkakati huu tutautekeleza katika mikoa yote vilipo viwanda vyetu”. Alisema Bwana Gadzios.
Wageni waalikwa waliofika kusherekea muonekano mpya wa kinywaji cha Coca-Cola.
No comments:
Post a Comment